aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 8, 2014

BONGO MUVI SIYO SKENDO, MAKUNDI, VISASI!

Uongozi wa Bongo Muvi, kutoka kulia: Katibu Mkuu, William Mtitu, Mwenyekiti, Steven Mengere a.k.a Steve Nyerere, Katibu Msaidizi Bi. Devotha Mbaga, Mweka hazina Mkuu, Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni katika picha ya pamoja baada ya kuchaguliwa.
KWENU,
Uongozi mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity ‘Bongo Muvi’. Kwanza hongereni kwa kuchaguliwa na bila shaka mtaanza kazi kwa nguvu zaidi huku mkisaidia kuifanya tasnia iendelee kuwa juu.
Mwenyekiti mpya wa Bongo Muvi, Steve Mengele Nyerere akizungumza.
Ndugu zangu, mna changamoto kubwa. Mna mambo mengi ya kuweka sawa katika klabu yenu. Sitaki kuzungumzia sana kuhusu udhaifu wa uongozi uliopita au kabla ya huo lakini nitajaribu kushauri kwa jumla kwa lengo la kuwasaidia.
Siku zote nimekuwa mkweli, sina ninachohofia katika kutetea masilahi ya sanaa na wasanii wa Tanzania. Kukataa ukweli ni sawa kukimbia kivuli chako mwenyewe.
Turudi kwenye hoja; mambo mengi machafu yalitokea kwenye klabu yenu kwa nyakati tofauti katika vipindi vilivyopita. Bongo Muvi ikawa kama genge la watu kukutana na kufanya yao kisha kila mmoja kuchukua time!
Siyo sawa. Naamini lengo la mtoa wazo wa kwanza kuhusu kuanzishwa kwa klabu hiyo, lilikuwa ni kuweka chombo cha kukutana kubadilishana mawazo, kusimamia na kutetea haki za wasanii. 
Bila shaka ilikuwa hivyo.
Lakini kipindi kilichopita, yametokea mengi, mpaka viongozi wengine walihusishwa kwenye skendo mbalimbali. Hivi jamani, kama kiongozi anakumbwa na skendo, anaweza kushughulikia nidhamu ya wanachama wake kweli?
Ikiwa yeye ndiye kinara wa tabia za hovyo, anaweza kuwasimamia wengine na kuwaonya? Bila shaka haiwezekani.
Kuna wakati wanachama walifungiwa uanachana na ushiriki wa filamu bila sababu za msingi, lakini minong’ono ikadai kuwa kulikuwa na visasi. Mara zote visasi husababishwa na uwepo wa makundi.
Fulani ana kundi lake na anamsikiliza fulani na wengine nao wakawa na makundi yao. Ndugu zangu, kufanya hivyo hamuwezi kujenga hata siku moja. Zikeni yote yaliyopita, sahauni yote, mtulie na mjenge Bongo Muvi mpya.
Nawaamini sana wote mliochaguliwa. Steve Nyerere (Mwenyekiti) ni jembe. Yuko kwenye game muda mrefu, anajua kero za wasanii, atumie nafasi yake vizuri. Dk. Cheni (Makamu Mwenyekiti) anajitambua, labda aamue tu kuwaangusha wasanii makusudi!
Kichwa cha William Mtitu (Katibu Mkuu) kiko sawa. Ndiyo maana hivi karibuni aliamua kuachana na kunyonywa na Wahindi na kuanza kusambaza sinema zake mwenyewe. Hawa ni watu ambao wakitulia na kufanya kazi kama timu, kwa hakika wanaweza kubadili sura ya Bongo Muvi.
Kuna Cloud (Mweka Hazina) ambaye ni wa muda mrefu. Naamini huyu anaweza kuwa kinara wa kusimamia nidhamu, maana yeye mwenyewe ana status nzuri. Anajiheshimu na yuko mbali kabisa na skendo. Viongozi wengine wote ambao sijawataja hapa, naamini kwa kushirikiana mnaweza kufanya kitu kikubwa.
Simamieni maadili, msikubali kuitwa majina mabaya mitaani wakati mna nafasi nzuri. Kwanza hakikisheni ninyi mnakuwa mifano katika maadili kisha muwasimamie na wanachama wenu.
Msimwangalie mtu usoni, fanyeni kazi. Anayetibua na kwenda kinyume na katiba yenu, sheria ichukue nafasi yake.
Shirikianeni wote kwa pamoja kurudisha imani na wapenzi wenu. Naamini hatutasikia tena skendo, makundi, visasi wala chuki kundini. Upendo ndiyo uwe kiongozi wenu. Siwezi kuacha kusema ukweli.

No comments:

Post a Comment