aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, January 10, 2014

AL SHABAAB Wapiga Marufuku Raia kutumia Internet Nchini Somalia

Wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al-Qaeda, wamesema kuwa wamepiga marufuku raia wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti kutumia internet.
Wapiganaji hao wametoa onyo kwa kampuni zote zinazotoa huduma ya internet siku 15 kufunga biashara zao.
kampuni yoyote au mtu yeyote atakayepatikana akipuuza onyo hilo atajulikana kama mtu anayewafanyia kazi maaduzi zetu, na ataadhibiwa kulingana na sheria za kiislamu,” ilisema taarifa ya kundi hilo ambayo ilitumwa kwenye mitandao yake.


Wanamgambo hao hutumia sheria kali za kiisilamu katika maeneo wanayotawala na kuwakamata watu mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.
Kundi la Shebab zamani lilikuwa likitawala katika sehemu kubwa za Kusini mwa Somalia na Kati, lakini likaondoa wapiganaji wake baada ya kushindwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrikawanaopambana nao. Majeshi ya Afrika wakiwemo wanajeshi kutokaUganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.
Lakini mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya maslahi ya majeshi ya serikali na yale ya kigeni, yameondoa matumaini ya kunusuru taifa hilo kutokana na vita vya miaka mingi.

Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment