aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, July 26, 2013

Brandts aondoka Yanga, amfuata Guardiola


Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amelazimika kukiacha kikosi hicho kwa muda baada ya kuhitajika haraka nchini Ujerumani.
Safari hiyo ya Brandts, inakuja wakati ambao kikosi hicho kikiwa katika maandalizi makali ya msimu ujao, ambapo akiwa huko atakutana na Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola katika mafunzo maalum.
Brandts ameliambia gazeti hili kuwa, ataondoka nchini leo usiku na lengo kuu ni kwenda kuongeza ubora wa leseni yake ya ukocha katika mafunzo yatakayofanyika kwenye Jiji la Bremen, Ujerumani.
Amesema mafunzo hayo yatamuwezesha kuongeza ujuzi katika fani hiyo na yatachukua siku tano.
“Leseni yangu ilikuwa inakwenda ukingoni, lakini bahati nzuri nimepata ruhusa kutoka kwa klabu yangu kuhudhuria mafunzo hayo ambayo sasa yataiboresha zaidi leseni yangu nikiwa pamoja na Guardiola, naweza kurudi hapa wikiendi ijayo,” alisema Brandts na kuongeza:
“Nimelipia euro 4,000 kwa ajili ya kosi hiyo na pia nimepa euro 1,000 kwa ajili ya hoteli na gharama nyingine za kuishi kwa muda huo. Hivyo jumla nimelipa euro 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 11).
“Nimeacha programu ya mazoezi na kila kitu ambacho nilipanga kukifanya, kwa msaidizi wangu Freddy (Minziro), sina wasiwasi kwa kuwa naamini anaweza kufanya kila kitu kwa ubora.”
Aidha, Brandts ameshauri kuwa timu hiyo ikipata kambi nje ya nchi kabla ya kuanza kwa msimu, litakuwa jambo zuri kwake.

No comments:

Post a Comment