aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 31, 2013

DALADALA, BODABODA ZANGONGANA KAWE, JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI YA LEO

Wapita njia wakishuhudia ajali  iliyotokea asubuhi hii maeneo ya Kawe karibu na viwanja  vya Tanganyika Packers, jijini Dar es Salaam,  kati ya mwendesha pikipiki na gari aina ya Toyota Hiace.  Hakuna  aliyeumia katika tukio hilo mbali na pikipiki kuharibika.
Pikipiki ilivyoharibiwa baada ya kupambana na gari hilo.

MAPENZI YAUA


WAKATI Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani, mapenzi yamemuua kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni jijini Dar kwa kuchomwa visu.
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Ibra.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.
Sehemu ya waombolezaji.
“Siku ya tukio Kelvin alikutana na Fatuma, akamuanzishia vurugu akimuuliza sababu ya kumuacha yeye ili aolewa na Ibra. Vurugu ilikuwa kubwa, Fatuma akaamua kumuita Ibra ili amsaidie.
“Ibra alipofika ndiyo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili na ndiyo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo.
Marehemu Ibra enzi za uhai wake.
Baada ya tukio hilo inadaiwa Kelvin na Fatuma walikimbia hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamepatikana.
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera.
Kamanda Wambura alisema kuwa Kelvin ambaye anahusika na mauaji hayo anasakwa na jeshi la polisi.
Mbali na Kelvin pia  mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Waombolezaji wakiwa na simanzi.

Neymar ~ Debut on Barcelona ~ Lechia Gdansk vs Barcelona ~ 30-7-2013

MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUCHEZA MECHI NYINGI ZA KIMATAIFA - AHMED HASSAN AGHAIRI KUSTAAFU

Mchezaji mwenye rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kimataifa. 
Ahmed Hassan, ameamua kutostaafu kwa kuongeza msimu mmoja wa 
kuichezea klabu ya Misri Zamalek.

Kiungo huyo mwenye miaka 38, ambaye kwa sasa amejiuzulu kuichezea 
timu ya taifa ya Misri, atacheza kwenye michuano ya kombe la 
mabingwa wa Afrika nchini, klabuya Cairo ilisema kupitia taarifa
 yake rasmi. 

Huu ni msimu wake wa pili akiwa na Zamalek, ambaye alijiunga 
nayo akitokea kwa mahasimu wao Al Ahly mwaka jana.
Hassan anatambuliwa na shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuwa 
ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi za kimataifa, akiwa 
ameiwakilisha Misri mara 184 kuanzia 1995 mpaka 2012. 

Hassan, ambaye ana rekodi ya kushinda kombe la mataifa huru ya 
Afrika mara nne, lakini hajawahi kucheza kwenye michuano ya
 kombe la dunia, pia aliwahi kucheza soka nje ya nchi katika 
klabu ya Anderlecht ya Belgium na Besiktas iya Uturuki.

BAADA YA LIONE MESSI - SASA RAISI WA BAYERN MUNICH ASHTAKIWA KUKWEPA KODI


Wiki kadhaa baada ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi 
kutuhumiwa kukwepa kulipa kodi, sasa raisi wa mabingwa 
wa ulaya Bayern Munich Uli Hoeness ameshatakiwa kwa 
makosa ya kukwepa kodi, mwendesha mashtaka wa
 Ujerumani amethibitisha.

Imegundulika kwamba mnamo April mwaka huu, Uli, 61,
 alishindwa kulipa kodi ya kodi akaunti yake iliyopo 
nchini  Switzerland mnamo mwezi January, na sasa
 imethibitika ameshtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi.

"Mwendesha mashataka wa jiji la Munich II amekamilisha 
uchunguzi," taarifa rasmi ilisema.

"Mahakama ya makosa ya jinai ya mkoa wa Munich II 
sasa inasubiriwa kuamua kukubali au kukataa mashtaka hayo."

Msemaji wa klabu ya Bayern Markus Horwick aliiambia
 SZ kuhusu issue hiyo: "Hatutosema kitu chochote kuhusu suala hili."

MPIGAPICHA ANYANYASWA NA USALAMA WA TAIFA





Mpigapicha wa New Habari Anthony Siyame akidhalilishwa na askari wa Idara ya Usalama wa Taifa wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Thailand, Yungluck Shinawatra baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Julai 30 2013.
(Picha kwa hisani ya Selemani Mpochi) 
 
Cha ajabu ni kwamba wakati mpigapicha huyo akifanyiwa visa na kushindwa kufanya kazi yake kwa utulivu wanahabari wengine wa kigeni walipewa ushirikiano mzuri na kufanya kazi yao bila bughuza  kabisa.

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI ALIVYO MGALAGAZA Thailand kwa KO


Bondia Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa 

mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga Ekkalak Saenchan wa Thailand 
kwa KO raundi ya kwanza PICHA NAwww.superdboxingcoach.blogspot.com



Bondia Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake Australia kulia 


akinyooshwa akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia 
Ekkalak Saenchan wa 
Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni 
mwa wiki iliyopita 


Bondia Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake Australia 

akimsikilizia mpinzani wake baada ya kumtwanga kumi nzito na 
kuhesabilwa wakati wa mpambano wake ata hivyo mpinzani wake 
akuendelea na kufanikiwa kupata ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza.
picha kwa niaba ya Mtandao wa SUPER D

SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUBADILISHANA WAFUNGWA NA NCHI YA THAILAND


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(kulia) pamoja 

na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Mhe. Sura Pong Tovichakehaikul (kushoto) wakisaini Mkataba wa kubadilishana Wafungwa
 kati ya Tanzania na Thailand.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja

(wa tatu kushoto) akiwa pamoja na Viongozi wengine Waandamizi wa
 Serikali ya Tanzania na Thailand wakishuhudia kusainiwa kwa Mkataba 
wa kubadilishana Wafungwa kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand jana.
 Julai 30, 2013 Ikulu, Jijini Dar es SalaamKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir 
Minja(kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati
 na Madini, Mhe.
 Stephen Masele walipokutana jana Julai 30, 2013 Ikulu, Jijini 
Dar es Salaam kushuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa kubadilishana
 Wafungwa kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand(Picha na Lucas
 Mboje wa Jeshi la Magereza).

VIDEO: Comedian anayefanana na Obama afanya utani kuhusu ziara ya Tanzania


Comedian anayefanana na Obama afanya utani kuhusu ziara ya Tanzania

Waziri wa kwanza Mweusi wa Italia atupiwa ndizi wakimfananisha na ngedere.


Italian Minister for Integration Cecile Kyenge gestures during a news conference in Rome June 19, 2013. REUTERS/Tony Gentile
Italia bado imendelea kukumbwa na wimbi kubwa la ubaguzi wa rangi pale Waziri wa Kwanza Mweusi alipotupiwa ndizi alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Chama.
Waziri wa Ushirikiano ni Mwitalia wa kwanza mweudi aliyeteuliwa hivi karibuni na amekuwa akipata taabu sana kutokana na dhana ya ubaguzi iliyojengeka miongoni mwa raia wa Italia. Cesile Kyenge ni mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye amekuwa akipigania haki ya wahamiaji kupata uraia wa kudumu wa Italia.
Muda mfupi kabla ya tukio hilo siku ya Ijumaa, wanachama wa mrengo wa kulia Forza Nuova waliandamana wakipinga kampeni ya Waziri Kyenge ya kutaka kumpa uraia mtu yeyote isipokuwa aliyezaliwa katika ardhi ya Italia.
“Uhamiaji Unaua” viliandikwa baadhi ya vipeperushi ambapo ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya Forza Nuova wakimaanisha kuwa mauaji mengi yaliyofanyika Italia yalisababishwa na Wahamiaji.
Ingawa ndizi alizokuwa akitupiwa zilimkosa, Waziri Kyenge alijibu katika mtanda wa kijamii wa twiter “sad” huzuni kwa kutupa chakula hasa katika wakati huu wa mgogoro wa kiuchumi.
“Ujasiri wa kubadilisha hali ya mambo unatoka ndani mwa mtu” alisema waziri Kyenge.

Hata hivyo, Waziri Kyenge amekuwa akikabiliwa na matusi mara kwa mara hata kutoka kwa wanasiasa wengine. Mapema mwezi huu, Mbunge mwanamizi wa kaskazini anayepinga sheria ya uhamiaji alimtukana matusi na kumlinganisha na “orangutan” Hata hivyo aliomba msamaha baadaye

List ya waigizaji wa Hollywood na mastaa wengine maarufu duniani ambao asili yao ni Nigeria.




Nigeria-flagNigeria ni nchi ambayo inafanya vizuri kwenye 
\upande wa entertainment  Africa, lakini kuna 
wasanii maarufu ambao wanafanya vizuri kwenye
 burudani huko Ulaya na Marekani asili yao ni 
Nigeria. Hawa hapa ni mastaa saba ambao ni 
wanaigeria lakini wanafanya vizuri kwenye 
movie na muziki kwenye mabala ya 
Ulaya na Marekani.
2
JACOB TAIWO CRUZ – TAIWO CRUZ
Taiwo Cruz ni mwimbaji anayefanya kazi zake 

Ulaya hasa nchini Uingereza, huyu jamaa 
kazaliwa kwa baba mwenye asili ya 
\Nigeria kabisa na mama mwenye asili
 ya Brazil. Taiwo Cruz alianza kuimba 
akiwa na miaka 12 na katika career yake
 ya muziki ameweza kushinda tuzo
 kadhaa kama BRIT awards,ASCAP 
awards,American Music Awards,
Billiboards music awards na
 nyingine nyingi. Hata jina lake
 la Taiwo lina asili ya Kiyoruba na 
mara nyingi hupewa kwa mtoto wa 
kwanza kuzaliwa kama wamezaliwa mapacha.
6
LEMAR OBIKA  - LEMAR
Lemar alizaliwa Tottenham  kwa  baba na 

mama wanigeria kutoka Enungu kusini 
mwa Nigeria, Lemar anajulikana kwa
 kazi yake ya usanii kwa uimbaji mahiri
 wa RnB,mwandishi wa nyimbo na
 producer. Mashabiki wengi wa 
msanii huyu hasa wanaigeria, 
hawakufahamu kamaLemar ana asili ya Nigeria.
1
HUGO WEAVING
Actor aliye-act kama agent Smith kwenye  

movie ya Matrix ni mnigeria.Jama
a huyu alizaliwa 
UCH(Univeristy College Hospital in Ibadan). 
Hugo akiwa na miezi 12 wazazi wake
 walihama Nigeria na kuhamia nchi 
nyingine.Hivi sasa mnigeria huyu 
anafanya vizuri huko Hollywood.

3
RICHARD AYOADE
Ayoade  kazaliwa na baba mnigeria na mama

 mnorway.Richard ni comedian maarufu huko
 Ulaya na mwaka jana alipata nafasi ya 
kuigiza kwenye movie ya Hollywood 
inayoitwa The Watch.Jina lake la mwisho 
Ayoade ni jina maarufu sana kwenye 
kabila la Yoruba
4
DONALD FAISON
Muigizaji huyu ni maarufu sana huko

 Hollywood,amezaliwa na baba kutoka 
nigeria na mama mwenye asili ya kimarekani.
5
DYLAN KWEBANA MILLSY
Anaitwa Dizzle Rascal Dizzie

 (Dylan Kwebana Mills) ni moja ya 
marapper wanaopewa heshima sana 
huko Ulaya.  Dizzle  aliwahi kushinda 
tuzo ya BET Act  mwaka 2010 na pia 
alifanya perfomance kwenye sherehe za 
ufunguzi wa Olympics huko London.
7
TYLER OKNMA – TYLER THE CREATOR
Huyu jamaa ni maarufu kama 

“The Black Eminem”. Japokuwa 
anasema kwamba hajawahi kukutana
 na baba yake,Tyler ana asili ya Nigeria
 kwasababu baba yake alikuwa mnigeria
 wa Igbo. The Black Eminem ambaye 
ni kiongozi wa kundi la 
“Odd Future Wolf Kill Them All”, 
amewahi kutoa album kadhaa lakini 
“Bastard” ndiyo album yake maarufu
 yenye mistari ya utata kupita kiasi 
ndio maana akaitwa Black Eminem.

MAMA WA JOHN TERRY AKESHA BAA

LONDON, ENGLAND

MAMA mzazi wa beki wa kati wa Chelsea, John Terry, Sue, amekutwa akiwa amelewa chakari na kuuchapa usingizi katika siti ya nyuma ya teksi aliyokodi baada ya kuzidiwa na pombe alizokunywa usiku kucha katika baa moja jijini London.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 55, alipanda ndani ya teksi hiyo saa 9 za alfariji akiwa ametoka kuponda raha na mkwewe, mke wa Terry, Toni.
Kwenye teksi hiyo, bibi Sue alitangulia kupanda na kwa sababu alichoka, aliamua kuangusha usingizi katika siti ya nyuma akimsubiri Toni atoke ili warudi nyumbani.
Tukio hilo la ulevi wa mama huyo, limekuja siku chache baada ya baba mzazi wa mwanasoka huyo kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubaguzi.

MBONI AANGUA KILIO MBELE YA MZEE RUKSA

 HOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha Runinga cha EATV,  Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji huyo alimwaga machozi wakati akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na kutoa shukrani zake kwa wote waliomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye
furaha kwa kumtambulisha baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo kwa mama yake.Aidha, mtangazaji huyo alimwita mama yake, bila ya kutarajiwa akaanza kumuomba msamaha mzazi wake huyo kwa kumsumbua na kumuahidi kwamba amejirekebisha.
“Nakuomba msamaha mama yangu, Mboni si yule tena nimebadilika, nisamehe sana,“ alisema Mboni kisha akaangua kilio kujutia makosa yake.
Baada ya tukio hilo, Mboni alisikika akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili ampe mume mwema. Mtangazaji huyo alirudia mara kwa mara kipengele hicho cha kuomba mume kiasi cha baadhi ya wageni waalikwa kusema kwamba ni kweli anahitaji mume kwani umri wake unahitaji kuwa na familia.Mbali na matukio hayo, Mboni alitambulisha vituo viwili vya watoto yatima ambavyo anavihudumia kupitia kampuni yake ya The Mboni. Mbali na Mwinyi wageni wengine walikuwa ni Shehe wa Mko wa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Asha Rose Migiro pamoja na Khadija Mwanamboka.
Wengine ni Shay-rose Bhanji na baadhi ya wanamuziki wa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Steve Nyerere na watu wengine maarufu.
NA GLOBAL PUBLISHERS 

VIONGOZI WAFUNGIWA GHALA LA KOROSHO NA KUMWAGIWA UPUPU MTWARA...


Mmea wa upupu shambani.
Viongozi wa Chama cha Msingi cha Ushirika wa Mazao na Masoko
 Lenganelo na Diwani wa Mchemo, Mshamu Chituta, wamekamatwa na 
wanachama, wakafungiwa katika ghala la korosho na kumwagiwa upupu.

Akizungumzia kisa hicho katika Baraza la Madiwani juzi, Diwani huyo 

alisema wanachama hao walishikwa na hasira mkutanoni, baada ya 
kudanganywa, ndipo walipomkamata  yeye na uongozi wa chama hicho na 
kuwafungia kisha kuwamwagia upupu.
Alitaja wenzake waliopata adhabu hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho,

 Hassan Nakuya, Katibu aliyemkumbuka kwa jina moja la Mnali na msaidizi 
wake, Ramadhani Mpanga.
Chituta alisema uongozi wa chama hicho, uliwatangazia wananchi kwenye 

mkutano huo, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magalla,
 angekuwapo.
Habari kutoka eneo la tukio, zilieleza kuwa viongozi wa chama hicho

 walitumia jina la Mkuu wa Wilaya kuitisha mkutano wa wanachama, ili 
kuwavuta wahudhurie kwa wingi.
Diwani Mshamu alisema hakuwa anajua kama uongo ulitumika, kwa kuwa

 siku ya tukio alikuwa na kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, lakini 
aliombwa na Katibu wa Chama cha msingi, asitishe kikao hicho na aende
 kwenye mkutano wa chama ambao pia ungehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya.
Kwa mujibu wa diwani huyo, wanachama waliitika mwito lakini mkutano 

ulianza bila Mkuu wa Wilaya, wakagundua kudanganywa ndipo wakaamua 
kuwaadhibu viongozi na yeye kwa kuwafungia ghalani na kuwamwagia 
upupu.
Alisema walijaribu kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya, ili afike kuwanusuru,

 lakini simu yake haikupatikana hivyo wakakaa ghalani kwa saa kadhaa,
 mpaka walipomtafuta  Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), aliyefika 
kuwafungulia.
Kutokana na malalamiko hayo ya Diwani katika Baraza hilo ambalo Magalla 

pia alihudhuria, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Newala, Ashidi Ndembo, 
alimwomba Mkuu wa Wilaya, kutoa ufafanuzi wa suala hilo, ili kuondoa hali 
ya sintofahamu baina ya diwani na uongozi wa chama cha msingi.
Akijibu hoja hizo, Magalla alisema hakuwa na taarifa na mkutano huo na 

kwamba siku inayotajwa kufanyika mkutano huo, alikuwa kwenye kikao cha
 Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa, mjini Mtwara.
“Nataka nichukue nafasi hii kueleza kwamba sikuwa na taarifa ya mkutano 

huo, siku hiyo nilikuwa katika kikao mjini Mtwara na simu nilizima kutwa 
nzima. Nilipoiwasha, nilikuta ujumbe kutoka kwa mtu nisiyemjua, nilipopiga 
simu nikagundua ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Lenganelo,”
 alisema Magalla.
Alisema baada ya kumpigia, Mwenyekiti huyo alimfahamisha kuwa alikuwa 

amefungiwa ghalani na wakulima na alimpigia kutaka msaada lakini simu 

haikupokewa, ingawa walishafunguliwa.
Magalla alionya wanaotumia jina lake kuitisha mikutano ya wananchi kwa 

kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria na utovu wa nidhamu, alitaka 
wahusika wa jambo hilo waache kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa
 dhidi yao.
“Nimesikitishwa sana na kitendo hiki, hasa ninaposikia kinafanywa na 

viongozi wenzangu. Kwa kweli si jambo jema…tunajua kuna baadhi ya 
maeneo wananchi wamekuwa hawajitokezi wanapoitwa katika vikao na 
mikutano, sasa kama viongozi wa eneo hilo wanahitaji msaada wa DC, ni 
vema wakawasiliana nami na kwa kuwa huo ni wajibu wangu nitakuja,” 
alisema Magalla.

USHAWAI FAHAMU KUHUSU HILI???


Baada ya Watanzania kukamatwa na dawa za kulevya, hiki ndio kimemkuta Madee akiingia Afrika Kusini






1
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com 

Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati 
anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita 
ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, 
uzito wa tukio la wale Watanzania wawili 
wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja 
cha ndege Johannesburg 
wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege,
 kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya
 kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa 
na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia 
Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport
 kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu
 dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, 
kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi
 wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue 
t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo
 nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake

 aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, 
Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa 
sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama 
dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio 
kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye
 foleni wanaposimama watu ila 
kwa pembeni kidogo, ni 
sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana 
na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee 
anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati 
wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana 
msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la 
TipTop Connection walimuomba radhi baada ya
 kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika 

kulivuruga sana begi lake.

2

                                                            SOURCE MILLARD AYO

MWALIMU AFUMWA CHINI YA KITANDA CHA MWANAFUNZI WAKE WA KIKE...!!



Mwalimu wa somo la Hisabati amebambwa akiwa amejificha chini ya kitanda cha mmoja wa wanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16.
Mwalimu huyo ambaye hakutajwa jina, mwenye miaka 35, aligundulika pale mama wa binti huyo aliporejea nyumbani kumtazama binti yake katika siku ya mwisho ya muhula.

Alikamatwa na Polisi wa Greater Manchester kwa tuhuma za kutumia vibaya nafasi yake ya uaminifu kisha akaachiwa kwa dhamana lakini amesimamishwa kazi.

Mama huyo aliwabamba wawili hao katika chumba cha binti yake baada ya kurejea kwenye nyumba ya familia iliyoko Bolton, Manchester, katika siku ya mwisho ya binti huyo ya muhula.

Chanzo kimoja kilieleza: "Wawili hao walirejea nyumbani kwa binti huyo sababu walijua hakuna yeyote angeweza kuwapo pale.

"Lakini mama huyo alikuja nyumbani mapema kuliko ilivyodhaniwa na kuwabamba.

"Alikwenda chumbani kwa binti yake na kukuta mwalimu huyo akiwa amejificha chini ya kitanda. Ulikuwa mshituko mkubwa. Mama huyo alipagawa."

Mwalimu huyo ameachiwa kwa dhamana na polisi hadi Agosti 15. Haikufahamika kama amesimamishwa na shule yake.

Msemaji wa Polisi wa Greater Manchester alisema: "Polisi wa Greater Manchester wanafanya uchunguzi baada ya mwanaume mmoja kuwa amekutwa kwenye chumba cha msichana wa miaka 16.

"Ijumaa, Julai 19, polisi waliitwa sehemu fulani katika eneo la Bolton kufuatia kuhusiana na ustawi wa binti wa miaka 16 ambaye anaishi katika sehemu hiyo.

"Maofisa walifika na baadaye siku hiyo mwanaume mwenye umri wa miaka 35 alikamatwa kwa tuhuma za kukiuka maadili ya nafasi yake.

"Ameachiwa kwa dhamana hadi Agosti 15, mwaka huu akisubiria hatua zaidi.

"Maofisa Polisi wa Greater Manchester na taasisi kadhaa katika eneo la Bolton wanachunguza mazingira yaliyochangia tukio hilo. Uchunguzi huu pia utatazama mambo yoyote ya ulinzi ambayo yanahitaji kujadiliwa na kuona kama kuna makosa yoyote yametendeka."

Tukio hilo limekuja takribani mwezi mmoja baada ya mwalimu wa shule aliyeoa, Jeremy Forrest kufungwa jela miaka mitano na nusu na Mahakama ya Lewes kwa kuteka mtoto mmoja baada ya kutoroka kutoka Ufaransa na mwanafunzi wa miaka 15.

Muathirika wake, sasa miaka 16, ameshikilia msimamo wa kubaki upande wa mtuhumiwa na wawili hao wamepanga kufunga ndoa mara atakapoachiwa kutoka gerezani
.

ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI...!!

 
Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
 
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...

  Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui. 

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...

"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho


IDD AZZAN ASEMA YUPO TAYARI KUNYONGWA HADHARANI ENDAPO ATAKUTWA NA HATIA YA KUUZA MADAWA YA KULEVYA...!!

 


Wakati Jeshi la Polisi likitoa visingizio kwamba linashindwa kunasa watuhumiwa wanaosafirisha dawa za kulevya wanaopitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kutokana na kukosekana kwa vitendea kazi, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kupigwa risasi au kunyongwa hadharani kama itathibitika anahusika na biashara hiyo.

Azzan alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One kuhusu kuwapo kwa madai ya barua iliyoandikwa na Mtanzania aliyefugwa Hong Kong nchini China akimtaja kuhusika na biashara ya dawa hizo.

Alisema hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara ya dawa za kulevya au biashara yoyote haramu na kwamba taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao ya kijamii ni za upotoshaji na zimetolewa kwa lengo la kumchafua.

 “Nimejipeleka polisi kwa mara nyingine tena na nimewaomba wafanye uchunguzi wa kina na kama nitabainika nahusika na biashara hiyo niko tayari kupigwa risasi hadharani, lakini pia sitendewi haki kwa wale ambao wanazusha jambo hili wachukuliwe hatua za kisheria,” alisema.
 Azzan aliongeza kuwa hayupo juu ya sheria hivyo ikithibitika kuna mtu anamtuma dawa za kulevya kupitia bandari fulani pia atakuwa tayari kuwekwa hadharani na kunyongwa maana atakuwa hafai kuendelea kuwapo Tanzania.

Alisema makundi yanayomwandama ni ya kisiasa kwa lengo la kutaka kumdhoofisha katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Mahojiano kati ya Azzan na radio yalikuwa kama ifuatavyo;

RADIO: Mhe Idd Azzan wewe ni mbunge wa Kinondoni inaelezwa kuwa wewe ni mmoja kati ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na mmekuwa mkipokea mizigo kupitia maboti makubwa yanayotoka Pakistan yanayopitia Bagamoyo, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam, hebu tujuze na wajuze Watanzania hili lina ukweli gani.

AZZAN: Hata mimi nimesikia hilo na bahati nzuri nimesoma kwenye mitandao kadhaa imeandika hivyo na kuna barua inayodaiwa kuandikwa na mfungwa mmoja ambaye amedai mimi ndiye nahusika kumtuma yeye.
 Napenda kuwajulisha Watanzania sihusiki kwa namna yoyote ile na biashara ya dawa za kulevya na siyo dawa za kulevya tu lakini pia biashara yoyote haramu sijawahi kufanya katika maisha yangu.

Niseme tu kuwa hizo ni taarifa ambazo zimetolewa kwenye mitandao ili kuaminisha watu hivyo, lakini kimsingi sihusiki na sijihusishi na biashara ya namna hiyo.

Baada ya kuziona habari hizi kwenye mitandao nilichokifanya na sababu ilishawahi kujitokeza tena na viongozi wangu wa CCM walishawahi kuyasema hayo kwenye mkutano wa vijana nikawaambia polisi wachunguze ili kupata ukweli wa hilo jambo.

Kama itabainika nahusika basi nichukuliwe hatua za kisheria mimi siyo Mungu wala sipo juu ya sheria, nimefanya hivyo kwa maana ya kuongea na Jeshi la Polisi nimejipeleka nimetoa maelezo na nimewataka polisi kwa sababu ni kazi yao wafanye uchunguzi wa kina, pili kama nahusika na tuhuma hizo hatua za kisheria zifuatwe dhidi yangu na kama siyo kweli hao wanaoeneza uzushi huo pia wachukuliwe hatua.

 RADIO: Unadhani kwa nini Mtanzania aliyeshikiliwa Hong Kong amekutaja wewe kuhusika na biashara hiyo?

AZZAN: Kwanza mimi siamini kwamba kuna Mtanzania anayeshikiliwa Hong Kong ambaye amenitaja mimi, sababu hiyo biashara kwanza sijawahi kuifanya, mimi niliiona hiyo barua haina jina la huyo Mtanzania mnayemsema, wala hakuna namba ya mfugwa sasa mfungwa anatakiwa kuwa na namba, asitaje jina ataje basi walau namba yake pia hakuna jina la gereza, kwa hiyo mimi siamini Mtanzania ambaye amefugwa kwa tuhuma za dawa za kulevya anitaje mimi kuwa nimemtuma. Hakuna hicho kitu na hakuna Mtanzania ambaye niliwahi kumtuma hicho kitu kimetengenezwa kwa nia ya kunichafua.

RADIO: Mheshimiwa unatafsiri vipi tukio hili?

AZZAN: Mimi ninachotafsiri tayari mapambano ya 2015 ndiyo yanaanza na watu wanatafuta jinsi ya kunichafua sababu hata tukienda kwenye kura nitawashinda, lakini si kutafuta mbinu chafu za kunichafua.

Yapo maneno ambayo nayazungumza bungeni hayawafurahishi wengine, lakini kwa Watanzania wengi yana manufaa, kwa hiyo kwa wale ambao hayawafurahishi wanaweza wakawa wamechangia katika kunichafua.

RADIO: Lakini Mheshimiwa Idd Azzan mara nyingi tu umekuwa ukitajwa na watu mbalimbali kwamba unajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya ama wewe ni mmoja kati ya watu wanaowaagiza watu mbalimbali kusafirisha mizigo hiyo ya dawa za kulevya hilo kwa upande wako unalizungumza vipi.

AZZAN: Nasema binafsi nimejipeleka polisi na nilishajipeleka mara ya kwanza baada ya kutokea tuhuma kama hizi, nikawaambia polisi wafanye uchunguzi kama nahusika nichukuliwe hatua za kisheria, nimekwenda tena kuwaambia polisi na nasisitiza polisi wafanye uchunguzi wa kina kama nahusika hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yangu.

Kama nitabainika nahusika na biashara hiyo niko tayari kupigwa risasi hadharani, lakini pia sitendewi haki kwa wale ambao wanazusha jambo hili wachukuliwe hatua za kisheria.

RADIO: Lakini Mheshimiwa kwa upande mwingine tayari taarifa zimeshatolewa kama hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, sasa endapo itabainika kweli umehusika ama hujahusika ni kitu gani ambacho utakifanya.

AZZAN:  Naomba niweke wazi kama itathibitika ninamtuma mtu madawa ya kulevya kupitia bandari gani mimi nipo tayari kuhukumiwa sababu sipo juu ya sheria na pia nipo tayari niwekwe hadharani waninyonge sifai kuendelea kuwapo Tanzania kama nahusika na hilo, na kama sihusiki serikali initendee haki kwa watu wanaosambaza uvumi huu nao wachukuliwe hatua siyo wakae tu na kumrushia mtu vitu vya uongo.

Awali Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Deusdedit Kato akihojiwa katika kipindi hicho juu kwanini JNIA umeonekana kuwa kitovu cha kupitishia dawa za kulevya, alisema sababu kubwa ni kwamba kuna tofauti kati ya nchi na nchi katika masuala ya teknolojia katika kubaini dawa za kulevya.

Kamanda Kato alisema nchi nyingine wana vifaa vya kisasa zaidi na kwamba wakati sasa umefika kwa serikali kuwekeza katika kupata vitendea kazi zaidi ili kufanikisha mapambano ya dawa za kulevya.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakishirikiana na viwanja vingine vya nchi mbalimbali kwa kubadilishana taarifa lengo likiwa ni mapambano ya biashara hiyo.

“Kimsingi wanaokamatwa wanakuwa ni wabebaji tu na siyo matajiri wa dawa za kulevya, bahati mbaya wabebaji wamekuwa wagumu sana kutoa ushirikiano kwa polisi, nasisitiza vitendea kazi vinachangia kuponya mtu asikamatwe nchini na kwenda kukamatwa nje,” alisema.

 Kamanda Kato alisema katika kipindi cha miezi sita hadi nane watu 14 wamekamatwa wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya nchini.

•Julai 5, mwaka huu wasichana wawili, Agnes Jerald (25) na Melisa Edward (24), walipita JNIA na shehena ya dawa za kulevya kilo 150  na walikamatwa Afrika Kusini na kushtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.
 Hawa walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakiwa na shehena ya dawa hizo aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8.

•Ijumaa wiki iliyopita yaani Julai 26, mwaka huu, Watanzania wengine wawili, walikamatwa Hong Kong wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine zenye thamani ya Sh. bilioni 7.6 akiwamo mmoja aliyekamatwa akitokea Dar es Salaam kupitia Dubai hadi Hong Kong.

Taarifa kutoka Hong Kong za Ijumaa wiki iliyopita zinaeleza kwamba, maofisa ushuru wa Uwanja wa Ndege wa Hong Kong (HKIA), walimkamata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26 akitokea Tanzania na alikuwa na dawa za kulevya aina ya heroine kilo 1.6 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.5, kwenye mzigo wake wa mkononi.

•Siku hiyo hiyo jioni, maofisa hao walimkamata Mtanzania mwingine mwenye miaka 45 ambaye alipelekwa hospitali na kutolewa gramu 240 za dawa za kulevya aina ya heroine. Taarifa zaidi zilieleza kuwa Mtanzania mwingine mwenye miaka 28 alikamatwa akiwa na kilo 2.03 za cocaine.