aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 24, 2013

TRAFIKI FEKI AWAKWEPA MAPAPARAZI, ACHEMSHA

JAMES Hussein, mkazi wa Kimara, Dar alikuwa na wakati mgumu wa kukwepa kamera za mapaparazi zilizotua Mahakama ya Wilaya Ilala, jijini Dar juzi baada ya kufikishwa kwa kosa la kujifanya trafiki.
...Akijificha Waandishi wasimpige picha
Tukio hilo lilijiri mahakamani hapo Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa alikana mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce  Minde.
Trafiki feki huyo alitumia muda mwingi kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini alichemsha kwani kila alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele yake.
...Akingizwa ndani
Hali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana.
Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema mnamo Agosti 14, 2013, huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar, mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo za askari wa usalama barabarani akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hapa waandishi walimbamba
Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa rumande Segerea, hadi Septemba 5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili kwa shilingi milioni kumi na nne.

SOURCE:GPL

No comments:

Post a Comment