aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 27, 2013

DAWA ZA KULEVYA AINA YA 'METHAMPHETAMINES' ZENYE LADHA YA CHOCOLATE NA STRAWBERRY ZATENGENEZWA KUWAVUTIA WATOTO THAILAND!!

Dawa za kulevya aina ya ‘Methamphetamines’ zenye ladha ya chocolate na strawberry zatengenezwa kuwavutia watoto Thailand!  
Hali ya biashara inayoendelea kupigwa vita duniani kote ya dawa za kulevya inazidi kutisha baada ya watengenezaji wa dawa hizo kubuni mbinu mpya ya kutengeneza dawa za ‘Methamphetamines’ zenye ladha ya chocolate na strawberry kwaajili ya kuvutia soko la watoto wadogo huko Thailand.
drugs
Director wa ‘The Princess Mother National Institute for Drug Abuse Treatment’ ya Thailand, Viroj Verachai,amesema wamegundua kuwa watengenezaji wa ‘yaba’ wanajaribu kubadilisha bidhaa yao ili kukidhi soko la kundi lililolengwa (watoto).
Wanaharakati wa kampeni ya kupambana na dawa za kulevya nchini humo wamewaonya wazazi juu ya mkakati wa mbinu hiyo mpya ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya ‘Methamphetamines’ ambazo pia ni maarufu kama ‘Yaba’ nchini Thailand, kwa mujibu wa mitandao.

No comments:

Post a Comment