aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 28, 2013

BONDIA BOTHA ATUA NCHINI

Mgeni rasmi katika mpambano wa Kimataifa wa Ubingwa wa WBF Bondia Bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu Zamani, Francois Botha  katikati baada ya kupokelewa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo. Wengine kushoto ni Raisi wa TPBO Yassini Abdalla na Rais wa World Boxing Federation, Howard Goldbeg pamoja na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' . Mpambano wa Ubingwa wa Dunia wa chama hicho unafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuwakutanisha Mabondia Francis Cheka na Phil Williams wa Marekani Agosti 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila wa pili kutoka kulia akifuraia jambo na Francois Botha pamoja na Yassini Abdalla kulia.

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwafikisha wageni kwenye hoteli ya Southern Sun wa pili ni Rais wa WBF, Howard Goldbeg, Rais wa TPBO, Yassini Abdallah na mmoja wa majaji wa mpambano huo pamoja na Bondia bingwa wa Uzito wa Juu Duniani Francois Botha.
(PICHA NA SUPER D)

No comments:

Post a Comment