aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 29, 2013

QUEEN SUZY: MIMI NDIYO BABA, MIMI NDIYO MAMA....


MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii maridhawa ya Staa na Mwana? Lengo kubwa la kona hii ni kuweza kukupa maisha halisi ya mastaa ambao tayari wamejaliwa kupata watoto wao.
Tunafahamu ni jinsi gani wanawalea watoto wao wanapokuwa nyumbani.
Leo tunakutana na mnenguaji tegemeo ndani ya Bendi ya FM Academia,  Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ anayeishi Kinondoni, jijini Dar.
Queen Suzy amejaliwa kupata mtoto mmoja aliyempa jina la Jackson (8) aliyemzaa na mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior, ungana nami katika mahojiano niliyofanya naye:
Staa na Mwana: Basi mwenzako nilikuwa sijui kama una mtoto tena mkubwa hivi!
Queen Suzy: (Kicheko) mimi ninaye tena ni mbaba kabisa kama unavyomuona hapa.
Staa na Mwana: Unajisikiaje unapomuona mwanao amekuwa kiasi hiki?
Queen Suzy: Kwa kweli hata wewe hapo siwezi kukuelezea furaha yangu ukaielewa, ila kimsingi najisikia faraja sana hasa msichana kama mimi kuwa na mtoto.
Staa na Mwana: Kwa nini umesema msichana kama wewe, kwani kuna ugumu gani?
Queen Suzy: Hakuna ila wengi wao wanapenda usichana zaidi wakipata mimba wanazitoa, sasa nashukuru nimepata mimba nimezaa mtoto wangu na leo hii najivunia.
Staa na Mwana: Hongera kwa hilo, baba yake lakini anajitoa katika suala zima la matumizi?
Queen Suzy: Yaani kuhusu mambo ya baba yake kwa kweli siyajui kwani mimi ni kama baba na ndiyo mama. Namlea mtoto wangu mwenyewe na ninamfanyia kila kitu mwenyewe.
Staa na Mwana: Mwanao anaijua kazi unayoifanya? Anaipenda?
Queen Suzy: Anaijua na anapenda sana ninavyocheza, anajua mama yake niko kazini na si vinginevyo.
Staa na Mwana: Kazi yako ya kunengua ni ya kurudi usiku, huoni kama mwanao atakosa malezi ya msingi?
Queen Suzy: Ni kweli lakini mwanangu anasoma ‘boarding’ akiwa likizo, huwa napenda kwenda naye sehemu mbalimbali za michezo ya watoto.
Staa na Mwana: Unapokuwa mbali na mwanao kwa muda mwingi, huoni kama utatoa mwanya kwa mwanao kujifunza tabia mbaya.
Queen Suzy: Namshukuru Mungu kwa kuweza kunipa mtoto mwenye nidhamu na anajua baya na zuri.
Staa na Mwana: Unapenda mwanao akikua afuate nyayo zako?
Queen Suzy: Siwezi kumchagulia lakini akipenda ataingia kwenye muziki maana baba na mama wote wako kwenye muziki.
Staa na Mwana: Nakushuru sana kwa ushirikiano.
Queen Suzy: Karibu tena.

No comments:

Post a Comment