aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 28, 2013

PICHA,KUWA WAKWANZA KUONA MCHEZAJI WA YANGA CHUJI AKIPAMBANA NA POLISI KWA KUTAKA KUMPIGA REFA CHUMBANI KWAKE

Askari Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga,
 ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa 
na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga 
na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini 
Dar es Salaam, leo jioni. 

Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu
 kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani
 wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi. Mwamuzi
 huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+ 
kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David 
Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera 
wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa 
kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye 
alipuliza kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.

Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza
 kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, 
katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David
 Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju
 huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo. 

HUKO KWINGINEKO Matokeo ya mechi za leo ni:- 
Rhyno 0-Azam 2, Oljoro 0- Simba 1, Tanzania Prisons 0- JKT 3, 
Ruvu Shooting 1- Mbeya City 2, Mgambo Shooting 1- Ashanti Utd 0, Mtibwa Sugar 1- Kagera Sugar 0
 Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado, akiruka kuokoa
 moja ya hatari langoni kwake.
 Beki wa Coastal, Juma Nyoso (wa pili kushoto) akiondosha
 hatari, huku wachezaji wa Yanga, Hussein Javu (kushoto) na
 hamis Thabit, wakiwania mpira huo.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) 
akiwatoka mabeki wa Coastal.
 Mabeki wawili wa Coastal, wakimdhibiti David 
Luhende.
 Didier Kavumbagu, akishangilia bao lake sambamba 
na Simon Msuva. Katika mchezo huo mwamuzi alitoa kadi 
nyekundu kwa wachezaji wawili Simon Msuva na wa Coastal.
Askari Polisi wakilinda mlango wa Chumba alichoingia 
Mwamuzi wa mchezo huo baada ya kuona usalama wake
 matatani, ambapo Chuji alijaribu kupangua ngome hiyo ili 
kuufikia mlango huo bila mafanikio.
SUPHIANI MAFOTO BLOG

No comments:

Post a Comment