aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 31, 2013

PICHA: WASANII NA WAREMBO MBALI MBALI NAO WALIKUEPO KATIKA UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA LULU



UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.

Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.

“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.
Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.CHANZO http://mrokim.blogspot.com
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City

 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
 .... Walitunzana tu kivyao vyao...

 noti alizo tuzwa Jide...

 Rich Rich akimwaga noti
 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
 Furaha ilitawala

 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.

No comments:

Post a Comment