aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 27, 2013

ALIYEGEUZWA MTUMWA WA NGONO AANIKA 'UCHAFU' WA KANALI GADDAFI

Kanali Muammar Gaddafi aliamuru kutekwa kwa wasichana wa 
shule ambao baadaye walishikiliwa kama watumwa wa ngono
 kwenye eneo lake, kwa mujibu wa kitabu kuhusiana na dikteta
 huyo.


Msichana mmoja, aliyetajwa kama Soraya, alitekwa nyara wakati 
akiwa na umri wa miaka 15 na kushikiliwa kwa miaka mitano 
katika sehemu ya chini kwenye ngome yake yenye urefu wa maili 
sita nje kidogo ya mji wa Tripoli.

Anasema alibakwa ovyo-ovyo, kupigwa na kudhalilishwa kwa
 utaratibu wa takribani kila siku na kushuhudia udhalilishaji 
unaofanana na huo kwa wasichana na wavulana wengine.

Stori yake na nyingine za wengine ambao wanasema walibakwa
 na 
dikteta huyo zinasimuliwa kwenye kitabu cha "Gaddafi's Harem:
 The Story Of A Young Woman And The Abuses Of Power In Libya" kilichoandikwa na mwandishi wa kimataifa wa Ufaransa Annick
 Cojean.

Kitabu hicho kimeshauza zaidi ya nakala 100,000 tangu 
kilipochapishwa nchini Ufaransa mwaka jana na tafsiri ya 
Kiingereza itakuwa mitaani mwezi ujao.

Mwandishi huyo anasema wanaume na wavulana pia walibakwa 
na Gaddafi pia aliwashughulikia watu maarufu na wake za 
waheshimiwa kutoka nchi za nje.

Kwa mujibu wa uchunguzi wake, Annick anasema walinzi wa
 kike ambao wamezoeleka kumzingira Gaddafi, walikuwa ni 
mabibi zake ambao hawakuwa na uelewa wowote wa silaha.

Annick alichunguza matumizi mabovu ya madaraka ya Gaddafi
 baada ya kukutana na Soraya (ambaye jina lake limebadilishwa), 
ambaye alimsimulia stori yake ya kuhuzunisha.

Baada ya kupeleka maua, Gaddafi, ambaye alikuwa na watoto
 wanane, alimpapasa kichwa chake. Alisema hii ilikuwa ni ishara
 kwa mikakati yake kwamba alikuwa akimtaka kimapenzi.

Siku iliyofuata aliitwa kwenye ngome yake iliyoko kwenye eneo la 
urefu wa maili sita karibu na Tripoli, Bab al-Azizia, ambako alivuliwa 
nguo zote, kunyolewa nywele na kupelekwa kwa Gaddafi.

Alisema Gaddafi alikuwa amelala akiwa hana nguo kitandani na
 kujaribu kumbaka.

Pale alipokuwa akimsukuma ajinasue, Soraya aliondolewa na 
mkuu wa nyumba ya uharimu Mabrouka kwa ajili ya 'adhabu'.

Alinukuliwa kwenye kitabu hicho akisema: "Alinikamata mikono 
yangu na kunilazimisha kukaa pembeni yake kitandani. Sikuthubutu kumtazama.

"Alisema, "Usiogope. Mimi ni baba yako. Hivyo ndivyo unavyoniita, 
sivyo? Lakini pia ni kaka yake na mpenzi wako. Nitakuwa hivyo 
wakati wote kwa ajili yako. Sababu utakuwa ukikaa na kuishi na 
mimi milele."

Mwanafunzi huyo wa kike walipewa picha za ngono kutazama
 na aliwezeshwa kutazama Gaddafi akifanya mapenzi na wengine 
hivyo kumwezesha 'kujifunza'.

Wavulana na walinzi wa kiume pia walibakwa na dikteta huyo,
 kwa mujibu wa kitabu hicho.

Soraya kisha akaruhusiwa kwenda nyumbani mwaka 2009 lakini
 anasema ameitia aibu familia yake sababu alifanya mapenzi nje ya 
ndoa.

Alisema alijihisi yuko huru kutoka mikononi mwa Gaddafi baada ya 
kifo chake mwaka 2011 mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa 
wenyewe.

Kitabu hicho kinaelezea mahojiano na mwanamke mmoja 
ambaye alisafirisha wasichana hao kwenda kwenye makazi
 ya 
Gaddafi na waathirika wengine.

Annick pia anamtuhumu Gaddafi, ambaye alimuoa Safia Farkash,
 kutembea na wanafunzi na wake za waheshimiwa kutoka nchi 
za nje.

Wageni wa kike walikuwa wakipimwa damu mara kwa mara na 
manesi wa Gaddafi kuhakikisha hawakuwa na maradhi endapo
 angetaka kufanya nao mapenzi.

Marie Colvin, mwandishi wa Sunday Times aliyeuawa nchini 
Syria mwaka 2012, aliripoti kwamba nesi mmoja alimkabili 
akiwa na sindano wakati alipokuwa mjini Tripoli kufanya 
mahojiano na Gaddafi. Alikataa kutolewa damu

No comments:

Post a Comment