aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 29, 2013

INASIKITISHA:MTOTO MIAKA 7 ALEA FAMILIA,WAZAZI WAWAKIMBIA...MAJIRANI WALIA....


Na Imelda Mtema
WAZAZI ambao hawajajulikana walikotokomea wamewatelekeza watoto wao wanne wanaoishi Kata ya Bangulo, Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam, Amani lina mkasa wote.
Mazigira ya nyumba ya watoto hao ni ya kutoa machozi hata kwa mtu mwenye roho ngumu kama jiwe. Nyumba iko hivyo, pa kulala ni chini, wadudu kibao huku wakiwa hawajui hatima yao.
Majirani ndiyo waliowaibua watoto hao baada ya kubaini kuwa baba yao hajaonekana kwa miezi kadhaa nyumbani hapo hali iliyosababisha wengine kulia.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati,  Sarah Shija (7) ambaye ndiye anayelea familia hiyo kwa sasa, aliwataja wenzake, Kevin Shija (8), Babu Shija (5) na Brighton Shija (6).
Alisema  mama yao mzazi aliondoka nyumbani hapo miaka miwili iliyopita baada ya kutokea mzozo kati yake na baba yao na kwenda kusikojulikana licha ya kwamba siku hiyo walimsihi sana mama huyo asiondoke.
Sarah aliendelea kuweka wazi kuwa, baada ya mama yao kuingia mitini, baba yao ndiyo akawa kila kitu lakini kumbe  na yeye alikuwa na lake moyoni.
Alisema miezi minne iliyopita, asubuhi baba yao aliamka asubuhi na kuwaachia shilingi 5,000 na kiasi kidogo cha unga kwenye kiroba na kuondoka akisema angerudi jioni.
“Mara ya mwisho baba alipoondoka alituambia angerudi jioni, akatuachia shilingi elfu tano kwa ajili ya kununua mboga na vitu vingine,” alisema Sarah.
Sarah alisema tangu siku hiyo baba yao  hakurudi tena huku wao wakiwa wamebaki wenyewe na elfu tano aliyowaachia ikiwa imeisha.
Alisema hali hiyo iliwalazimisha kusimama masomo kutokana na ugumu wa maisha kwa sababu mara nyingi wanaamka asubuhi wakiwa na njaa hivyo kushindwa kuelewa kinachofundishwa na walimu.
“Tunalala na njaa, tunaamka na njaa, tunashinda na njaa sasa tusingeweza kwenda shule kwa sababu tunakuwa tunatetemeka mwili. Hatujui baba atarudi lini,” alisema Sarah na kuangua kilio.
Alisema imefika hatua nduguze wakishikwa na kiu anawapeleka kunywa maji machafu ya kwenye madimbwi ambayo pia yana chumvi kupita kiasi kwa sababu hawana  fedha (shilingi mia nne) ya kununua maji salama.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Sarah alimuomba baba yao  popote alipo kurudi nyumbani na kuendelea na maisha. Pia walimtaka mama yao akisoma habari hii akawachukue kwani maisha yao ni magumu sana na yeye analazimika kufanya shughuli nyingi za nyumbani ili kuhakikisha uhai wao haukatishwi na njaa.
Ili kujua maisha yao zaidi ya kusikitisha usikose kuangalia Kipindi cha Wanawake Live cha Mtangazaji Joyce Kiria ambacho kitaonesha ‘live’ maisha magumu ya watoto hao.
 
KUSAIDIA FAMILIA HII, TUMIA NAMBA HIZI: 0754 021 501 NA 0713 612 533

No comments:

Post a Comment