aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 28, 2013

VYOO VYA SHULE YA MSINGI UKANGE MAKETE NI MAJANGA....

Muonekano wa choo hicho kwa mbele kutokana na kukosa milango wamelazimika kutengeneza uzio wa nyasi.
 
Kushoto ndiyo tundu halisi la choo, na tundu la kulia limetokana na choo hicho kubomoka chenyewe.

 Nyufa zilizomo kwenye kuta za choo hicho.

=============================
Na Edwin Moshi, Makete.

Wanafunzi wa shule ya msingi Uganga kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani Njombe wapo hatarini kupoteza maisha yao kutokana na vyoo wanavyovitumia kubomoka na kuweka nyufa na matundu makubwa kutokana na uchakavu.

Mtandao huu umebisha hodi shuleni hapo hivi karibuni ka kukuta vyoo hivyo vinavyotumiwa na wanafunzi vikiwa katika hali mbaya huku wanafunzi hao wakiendelea kuvitumia bila wasiwasi.

Mwanafunzi mmoja anayesoma darasa la tano katika shule hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni amesema haoni shida kutumia vyoo hivyo kwa kuwa hakuna sehemu nyingine ya kujisaidia na kuongeza kuwa licha ya hatari ya kupoteza maisha waliyonayo wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo lakini bado wataendelea kuvitumia.

Akizungumzia suala hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Danie Kyando amekiri kuwepo kwa vyoo hivyo chakavu na kusema kuwa ameshapeleka kwenye ngazi husika suala hilo ambapo amejibiwa kuwa litafanyiwa kazi.

Amesema kwa hivi sasa wanamuomba Mungu isitokee hatari yoyote kwenye vyoo hivyo katika kipindi hiki wanaposubiri wakubwa kulishughulikia suala hilo kama walivyomuahidi ingawa ni muda mrefu umepita.

"Mimi katika taarifa zangu wakati mwingine huwa naandika kuwa shule haina vyoo vya wanafunzi kutokana na uchakavu hebu ona mwenyewe vyoo gani hivi, hii si hatari tupu, matundu mengine tumeziba na magogo ili wanafunzi wasiingie" alisema.

Shule hiyo ambayo inadhaniwa kuanza miaka ya 1970 inakabiliwa na changamoto lukuki ikwemo majengo kwa kuwa mengi yamechakaa.

No comments:

Post a Comment