aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 24, 2013

MONALISA ‘AOGESHWA’ SHAMPENI UFUKWENI

STAA wa filamu za Kibongo,  Yvonne Cheryl  ‘Monalisa’ amejikuta akiogeshwa shampeni na wafanyakazi wa Redio Times FM baada ya kumfanyia surprise katika fukwe za Coco, jijini Dar. 
Akizungumza na Weekly Exclusive Star, Monalisa alisema tukio hilo lilitokea juzikati ambapo alikuwa akitimiza miaka 32 lakini hakuwa akikumbuka kama ni siku yake ya kuzaliwa ndipo wafanyakazi wenzake walipompigia simu na kumtaka aende Coco Beach.
Alisema alipofika alishangaa kuwakuta wafanyakazi wenzake, wakiwa na shampeni ndipo zoezi la kumwagia shampeni likaanza hadi walipohakikisha ameloa chapachapa ndipo wakamwambia kuwa wamemuandalia pati.

“Nilipoitwa nilijua ni kampani ya kawaida, lakini nilipofika, nilishangaa kuona wamejikusanya na mmojammoja alinimwagia shampeni na waliokuwa hawana kinywaji hicho, walinimwagia maji,” alisema Monalisa.
Baada ya kumwagiwa vinywaji hivyo, wafanyakazi hao walianza kumuimbia huku wengine wakimkumbatia kwa ishara ya upendo na kumtakia maisha marefu ya amani na upendo.

 “Kweli namshukuru Mungu kunijalia afya njema na kuniwezesha kutimiza miaka hiyo kwani ni wengi ambao wametangulia mbele za haki mpaka sasa mimi bado napumua,” alisema Monalisa.
Mwishoni, Monalisa aliwashukuru watu wote waliompongeza pamoja na marafiki zake waliomuandalia ghafla fupi ingawa alitania kwa kusema, “Walikosa keki tu.” 

No comments:

Post a Comment