aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 21, 2013

MAMA WA BINTI KIZIWI AFUNGUKA,SAKATA LA KIFUNGO HONG KONG....

HATIMAYE mama mzazi wa Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi, amefunguka kuhusu madai kwamba mwanaye amenyongwa nchini Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
  Mama mzazi wa Binti Kiziwi, Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar.

Mama huyo aitwaye Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar, amesema kuwa mwanaye amefungwa miaka mitatu na nusu na anawasiliana naye kwa njia ya simu kila baada ya miezi miwili.
“Taarifa za mwanangu kunyongwa si za kweli bali amefungwa miaka mitatu na nusu,” alisema mama huyo.
Mama huyo amemtupia  lawama rafiki wa karibu wa Binti Kiziwi aliyemrubuni kufanya biashara hiyo ya kusafirisha madawa ya kulevya.
                 Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi.
 
“Sikuijua safari hiyo ya mwanangu ila nilipigiwa simu na rafiki yake wakiwa wameshafika Nairobi, Kenya,” alisema.
Kama vile haitoshi, mama huyo anamlaumu rafiki kwa kuchukua dola 5,000 za mwanaye alizokutwanazo wakati akikamatwa.
Mbali na kuwasiliana na mwanaye, mama huyo amesema Binti Kiziwi amekuwa akimtumia fedha licha ya kwamba yuko gerezani.
“Ananitumia fedha, anasema kuwa huwa wanafanya kazi wakiwa gerezani na kulipwa,” alimalizia.

No comments:

Post a Comment