aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 21, 2013

KISA CHA DIAMOND KUCHELEWA KUPANDA STEJINI MOMBASA NA MASHABIKI KUANZA KURUSHA CHUPA...

MBONGO FLEVA, Nasibu Abdul ’Diamond’ anayekimbiza na wimbo wake wa Kesho,  yamemkuta makubwa mjini Mombasa, Kenya alikokwenda kugonga shoo na kusababisha vurugu kubwa ukumbini. 
Nasibu Abdul ’Diamond’.
Cha kushukuru Mungu, Diamond hakusababisha vifo stejini wala madhara makubwa, lakini kuchelewa kwake kupanda jukwanai hadi saa 9:30 usiku kulizua vurugu kubwa na wapenzi kurusha chupa jukwaani.
Mashabiki waliokuwa wakihudhuria onesho lake walipandwa na jabza baada ya kuona muda ukienda bila ya staa huyo kuonekana jukwaani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Diamond alichelewa kupanda jukwaani katika Ukumbi wa Hoteli ya Mombasa Beach Resort kutokana na kutaka kutimiziwa madai yake.

Staa huyo ambaye hivi karibuni alipagawisha katika shoo ya Nairobi nchini humo, inadaiwa aliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya kukodi hadi Kenya kitu ambacho kiliwagharimu waandaaji wa shoo zake fedha nyingi.
Baada ya kufika Kenya alipiga shoo kali jijini Nairobi na kuwapagawisha Wakenya.
Hata hivyo, katika shoo ya Mombasa ndipo yalipotokea machafuko ya jukwaani.

Inadaiwa Diamond alikuwa akitaka kumaliziwa malipo yake na kutaka kulala katika hoteli na chumba chenye hadhi ya juu zaidi huku akikataa kukaa katika Hoteli ya Mombasa Beach Resort.
Hata hivyo, wenyeji wake walimtimizia vitu alivyotaka na staa huyo akapanda jukwaani saa 9:30 usiku.
Alipopanda jukwaani sambamba na wacheza shoo wake, Diamond alifunika kinomanoma na kuwafanya mashabiki kusahau kama alikuwa amechelewa kuanza shoo.

Kabla ya shoo haijafikia kikomo, Diamond alitoweka jukwaani. Hali hiyo ikazua tena kizaazaa cha kurushwa kwa chupa kiasi cha madansa wa staa huyo waliokuwa jukwaani kutafutana.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Diamond na kumuuliza kilichotokea ambapo alikiri kuchelewa kupanda jukwaani na madansa wake kuponea chupuchupu kupigwa na chupa.

“Nilichelewa, nilipanda jukwaani saa tisa na nusu usiku sababu ni waandaaji kugoma kunimalizia fedha zangu dola 6,700,” alisema.
Diamond alisema kuwa chupa zilirushwa kabla hajapanda jukwaani na baada ya kushuka kutokana na uchovu aliokuwa nao.
“Mara ya pili zilirushwa baada ya miye kuondoka jukwaani kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana na mashabiki wakagundua sikuwepo jukwaani ndipo balaa likaanza.

“Nilishuka jukwaani na kuwaacha viduku (wacheza shoo wake) wakiendelea na kazi yao ya kucheza sasa mashabiki walipogundua  kuwa sikuwepo jukwaani ndipo walianza tena kurusha chupa,” alisema Diamond.

No comments:

Post a Comment