aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 21, 2013

MAKAHABA NCHINI KENYA WAOMBA ULINZI WA POLISI WAKIWA KAZINI ILI NAO WALIPE KODI SERIKALINI

 
MAKAHABA nchini kenya sasa wanataka watambuliwe na wapewe ulinzi wanapokuwa kazini, ili na wao watoe kodi kwa serikali.

Kupitia chama chao, Africa Sex Workers’ Alliance (Aswa) wanawake hao wanasema kwamba biashara yao ni sekta ambayo inatoa fursa nzuri kwa nchi kujiendeleza kiuchumi.

“Tunataka watu watuangalie kama tunaoweza kusaidia kukuza uchumi huu na wala si kuangalia kwamba tunaendeleza mmomonyoko wa maadili. Biashara hii inaajiri mamia, kama si maelfu ya watu kote barani, akasema mkurugenzi wa chama hicho, Bi Doughtie Ogutu.

Alisema chama cha Aswa kilianzishwa kwa madhumuni ya kutetea maslahi ya wanachama ambao wamepitia mengi, yakiwemo kupigwa, kuuawa na hata kulazimishwa kushiriki ngono na wanyama miongoni mwa mengine.

Ingawa wanaamua kuendelea na biashara hiyo, makahaba wanakiri kwamba biashara hiyo ni hatari, hasa iwapo watapatana na wateja wabaya au hata katika hospitali wanazokwenda kutibiwa.

Bi Ogutu anakumbuka miaka minane iliyopita pale mmoja wao alipopata mteja Mzungu lakini akarejea akiwa maiti. Tena mwanzoni mwa mwaka huu, wasichana wakakamatwa katika eneo la Pwani wakiwa na mwanamume mwengine wa kigeni na kushtakiwa kwa kujihusisha na ngono isiyostahili - na mbwa.

“Hao wasichana hawakufanya hivyo eti kwa sababu walikuwa wakipenda. Walilazimishwa. Nilienda Mombasa kufuatilia kesi hiyo. Ni kwa sababu wanawake hawa hawalindwi na sheria. Wateja wao huwadanganya kuwa watawalipa, lakini wanapofika nao kwenye nyumba zao ambapo hakuna hata anayesikia ukipiga kelele, unafanya nini?” akauliza.

Kwa sasa, chama cha Aswa kinapanuka kutoka kuwepo katika mataifa kumi na kinaelekea Magharibi na Afrika ya Kati. Lakini ushawishi wake hapa Kenya umekumbwa na changamoto nyingi.
Maandamano

Mwaka jana mwezi Machi, tawi lake la Kenya Sex Workers Alliance (Keswa) liliandaa maandamano kwenye barabara za jiji la Nairobi kutaka wafanyakazi hao watambuliwe, ili wawe wakitozwa ushuru. Keswa walidai kuwa na wanachama 40,000 ambao wanaweza kuchangia pakubwa katika uchumi wa nchi hii.

Lakini kamati maalum ya Baraza la Jiji wakati huo, iliyoundwa na Meya Goerge Aladwa kuangalia kama kuna faida ya kuruhusu makahaba kuendeleza biashara yao, ilikataa mapendekezo ya wanawake hao.

No comments:

Post a Comment