aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

KASHFA NZITO! MAMA KANUMBA ADAIWA KUUZA MAGARI YOTE YA MAREHEMU MWANAE NA PESA KUNYWEA POMBE NA MAMA LULU!


Inavyosemekana imebaki Hice tu ambayo nayo kesha pewa dalali atafute Mnunuzi. Ofisi nayo inapumulia mashine. kuna mazito ndani ya familia hiyo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Xdeejayz imeibua tuhuma nzito toka kwa familia ya Marehemu Stiven Kanumba inayomtuhumua Mama wa msanii  Flora Mutegoha kuuza mali za mwanae kisha pesa kunywea pombe na mzazi mwenzake Mama Lulu huku akiisahau familia.
Habari za uhakika toka ndani ya familia hiyo zilisema kuwa Mama Kanumba hivi karibuni alianza kuiuza gari ya kifahali ya V8 na alimuuzia  shilingi milioni 30 Mama Salma Mtambo ambae ni mfanyabiashara maarufa Jijini Dar kisha pesaa hiyo kwenda kunywea pombe yote na kuisahau familia yake.


Aidha chanzo hicho kiliendelea kusema “ Haikupita muda tena ameuza gari nyingine aina ya Mark II kwa shilingi milioni 6 kisha kula bata pesa yote na sasa hivi ameshawapa madalali kazi ya kumtafuta mteja wa kuimalizi Hice aliyokuwa anaitumia marehemu kwa ajili ya kazi zake za Location” Alisema dada huyo ambae ni ndugu na Mama Kanumba na aliomba hifadhi ya jina lake kwa usalama wake.


Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa tangu mama Kanumba ashinde kesi ya mirathi hiyo ya mwanae amekuwa hana ushirikiano mzuri na baadhi ya ndugu zake “ Yani kweli pesa inabadilisha mtu huyu mama sisi ni ndugu yetu kabisa lakini tangu azitwae mali za mwanae basi hataki ushirikiano wowote na sisi kwa mfano zile pesa za rambirambi ya msiba milioni sabini akachukua milioni 50 akanunua nyumba maeneo ya Mbezi Temboni hilo tulimpongeza” Alisema bint huyo mdogo
Msichana huyo aliongeza kusema “ Lakini baada ya hapo mama huyu alikutana na Mama Lulu ambapo hali imekuwa mbaya ambapo wenyewe wameshauriana nini sijuia na walianza kuiuza ile V8 ambapo pesa yote walilia bata hadi ikaisha na hivi karibuni akaiuza gari nyingine ya marehemu aina ya Mark II na pesa hiyo wameitafuna yote hadi imeisha na sasa hivi anaimalizia ile Hice ambayo ndio ilikuwa tegemeo kwa ajili ya kampuni sijui tufanyaje jamani?” Alimaiza kusema bint huyo kwa uchungu.
Baada ya kupata taarifa hizo waandishi wetu walijaza mafuta gari ya ofisi na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama huyo  kwa ajili ya mahojiano na kufanikiwa kufika nyumbani kwa Mama Kanumba ambapo waandishi wetu wakiwa kamiri na kamera za siri aina ya Kalamu ambapo waligonga geti hilo jeusi na kufunguliwa na msichana ambae alijaitambulisha kwa jina la Husna ambae alisema kuwa yeye ni house girl na mara baada wanahabari wetu kijitambulisha na kuomba kuongea na Mama Kanumba msichana huyo alijibu kuwa Mama huyo alikuwa ametoka hivyo labda waandishi wetu warudi tena kesho yake au baadae.

No comments:

Post a Comment