aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

JINI KABULA NA ISABELA ACHENI UNAFIKI....!!


Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ na Isabela Mpanda katika pozi.

 KWELI aliyesema heri kumfadhili mbuzi kuliko binadamu ana maudhi, hakukosea. Hili limedhihirishwa na ninyi wasanii wa filamu na muziki Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ na Isabela Mpanda hivi karibuni baada ya kuonesha tabia ya kinafiki kwa kuropoka maneno ya kuponda  kwenye vyombo vya habari.


         Jini Kabula’ na Isabela Mpanda
Siku kadhaa zilizopita kuna habari ilitufikia kuhusu ninyi ambao ni marafiki kugombana na kutolewana maneno mbofumbofu ya kutukanana.
Cha kushangaza baada ya habari hiyo kuingia mitaani mlikimbilia runingani kufanyiwa mahojiano kwenye Kituo cha EATV ambapo mliulizwa kuhusu tofauti zenu lakini mkakana habari hiyo na kusema kuwa siyo kweli na yaliyoandikwa ni ya uongo ninyi ni marafiki na hamuwezi kutengana.
Isabela unatakiwa kubadilika kwa sababu tabia hiyo ya kinafiki siyo nzuri kwani ulitoa ushirikiano wote unaotakiwa kwenye habari hiyo lakini baadaye ulikuja kukanusha wakati unajua kabisa ulizungumza na kueleza jinsi ulivyomfukuza Jini Kabula nyumbani kwako. Je, uliona ukisema ukweli utapigwa na huyo rafiki yako au nini? Badilika wewe ni msanii na kazi zako bila mwandishi jamii haiwezi kukutambua.
Kwa upande wa Jini Kabula, nawe unahitaji kubadilika kwani kama kweli ulimtukana Isabela kwa sababu alikuambia mambo ya Jacqueline Pentzel kununua gari ulitakiwa ueleze mbele ya watazamaji ambao ni mashabiki wenu kuwa ni kitu gani kilitokea na siyo kukanusha kitu ambacho ni cha kweli.
Ni kweli wewe Isabela na Jini Kabula hampendani na urafiki wenu ni wa kinafiki kwa sababu kila mmoja akihojiwa anamkandia mwenzake. Ni kwa nini? Kwenye Kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, juzi wewe Jini Kabula ulikiri kujitoa kwenye Kundi la Scorpion Girls kutokana na kutoeleweka na sasa umeamua kufanya kazi kivyako kama ilivyokuwa kwako Isabela ambaye ulijiengua mapema na kutoa kazi yako mwenyewe ikiwa ni muda mfupi baada ya ninyi wawili kumtimua Jack Pentzel.
Ukweli tabia zenu za kubadilika kama kinyonga zinakera na kuchefua kwani mkiamka leo mnazungumza kingine kesho mnabadilisha na tabia hii imekuwa kwa wasanii wengi kwani wakishazungumza na waandishi wa magazeti na habari ikishatoka hukimbilia runingani au redioni na kuikanusha habari ambayo wenyewe mlitoa ushirikiano wa kutosha.
Jamani ninyi ni kioo cha jamii mnatakiwa kubadilika kwani tabia yenu hiyo siyo nzuri na mnatakiwa kuelewa kuwa kufanya hivyo siyo kwamba umaarufu unazidi bali thamani yenu inapotea, acheni hizo badilikeni ninyi ni watu wazima na siyo watoto! Mijimama na watoto wenu hamuoni aibu kuwa vigeugeu? For the love of game!

No comments:

Post a Comment