WANAFUNZI wa skuli mpya ya sekondari ya Mpendae wamelazimika kukatisha baadhi ya vipindi vya masomo, baada ya zaidi ya wanafunzi 10 kuchagawa jana.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:00 na saa 5:00 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Wanafunzi waliokutwa na mkasa huo ni wanawake wanaosoma kidatu cha pili na nne, hali iliyosababisha taharuki kubwa na kusababisha walimu kusitisha masomo.
Mwandishi wa habari hizo alipowasili skuli hapo alishuhudia makundi ya wanafunzi wakikimbia ovyo wengine wakirejea nyumbani.
Mwanafunzi mmoja wa kidatu cha nne, Subira Mgeni aliliambia gazeti hili kwamba tukio hilo limewaweka katika wakati mgumu na kusababisha kukosa vipindi muhimu.
Mwalimu Salim Mohammed Khamis, alisema chanzo cha tukio hilo ni kuwepo mazingira ya kishirikina huku baadhi ya wanafunzi kukiuka taratibu za misingi ya dini na hatimae wadudu waovu huwasumbua.
Alisema ni vyema wazazi kuwa makini juu ya uangalizi wa watoto wao wanapokwenda skuli kwa kuhakikisha wanafuata maadili na wanaepuka kutumia vifaa visivyostahiki ikiwemo kujitia manukato.
No comments:
Post a Comment