aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 15, 2013

UPDATE:MAAMUZI DHIDI YA MADIWANI NANE WALIOFUKUZWA YAKO PALEPALE,BI BUHIYE...


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Bi. Constansia Buhiye leo amesisitiza kuwa maamuzi yaliyotolewa na Halmashauri kuu ya Mkoa ya kuwafukuza na kuwaondolea nyadhifa madiwani wanane wa chama hicho Manispaa ya Bukoba yako palepale.

Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa CCM 
kuhusiana na Tamko la Katibu Mwenezi Taifa Ndugu Nape Nnauye la kutengua maamuzi ya Halmashauri kuu ya Mkoa wa Kagera, Bi Buhiye amesema hata taarifa ya Nape hajaisikia, na kwamba  maamuzi waliyoyafanya ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kagera akiongea na waandishi wa habari leo kusisitiza kuwa  maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa dhidi ya madiwani  wanane wa CCM  Bukoba yako palepale
  Waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera leo


No comments:

Post a Comment