aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

RONALDO: "SIJUI HATMA YANGU NDANI YA MADRID - MIMI SIO MTU SAHIHI KUZUNGUMZIA ADA YA UHAMISHO WA GARETH BALE KUJA MADRID"

Hatma ya Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid imezidi kuleta 
mkanganyikobaada ya mshambuliaji huyo kugoma kuthibitisha 
taarifa kwamba amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano.

Marca iliripoti kwamba mreno huyo amekubali kuongeza mkataba
 mpya wa kuendelea kubaki Bernabeu mpaka mpaka 2018, baada ya
 kuongezewa mshahara mpaka kufikia 17million euros (£14.8million) 
kwa mwaka baada ya kodi na piawamekubaliana na klabu kuzungumza
 juu ya mgawanyo mpya wa haki za taswira.  

Ronaldo bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake, lakini hivi 
karibuni amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea kuitumikia klabu 
yake ya Manchester United. 

Ronaldo alikaririwa akisema: "Sitothibitisha kitu chochote - 
nitaendelea tu kufanya kazi ambayo naifanya kila siku.  
"Hatma yangu ndani ya Madrid - Sijui itakuwaje. Kwa muda 
huu mie bado ni mchezaji wa Real, kuhusu kitachotokea huko
mbele sifahamu kwa kweli.   
"Ngoja tusubiri tuone nini kitatokea - lakini kwa sasa nipo sawa na 
mahala nilipo."
Ronaldo apia alizungumzia Gareth Bale na tetesi za usajili wake 
kwenda Real.
Madrid wanaaminika wapo tayari kulipa kiasi cha £95m ili kumpata
 Gareth Balelakini Ronaldo aliongeza: "Sitotaka kulizungumzia suala 
hilo kwasababu mimi sio mtu sahihi kusema kama anastahili kununuliwa
 kwa fedha hizo au la - au ni dili nzuri au hapana. Sitotaka kuzungumzia 
kuhusu wachezaji wengine."

No comments:

Post a Comment