aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 20, 2013

IZZO ATAMBA VIDEO YAKE IMEONGOZWA KUANGALIWA


MSANII wa muziki wa bongo fleva nchini, Izzo Bussiness ameweka wazi kuwa kutokana na ubora wa video ya nyimbo yake inayojulikana kwa jina la 'Love me' ndio sababu iliyopelekeea kuangaliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Izzo aliweka wazi kuwa tangu aanze kufanya muziki na kutoa video za nyimbo mbalimbali, video ya wimbo huu umekuwa ni miongoni mwa video zilizofanya vizuri ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu iachiwe.

Alisema kuwa tangu video hiyo ingizwe kwenye mtandao mwezi mmoja sasa haijapata 'comment' mbaya na imeweza kuangaliwa na watu zaidi ya elfu arobaini na moja.

"Nyimbo hii kwakweli inanipa hamasa kubwa ya kuendelea kufanya muziki kwani ni kipindi kifupi tangu tuiachie na imeweza kufanya vizuri katika gemu la muziki wa kizazi kipya imeongozwa kwa kupendwa na teyari imeshaanza kushika nafasi ya kwanza katika chati za muziki ya kibongo" alisema Izzo.

Aliongezea kuwa ujanja sasa ni kulisoma soko linataka nini na kutoa video yenye ubora huku ukizingatia mahadhi pamoja na mazingira ya nyimbo.

Alielezea kuwa moja ya sababu inayopelekea video hiyo kufanya vizuri ni kutokana na video hiyo kuchukua watu wachache, huku ikiwa imetengenezwa kwa umakini hali iliyopelekea muangaliaji asichoko kuangalia.

No comments:

Post a Comment