aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 23, 2013

HATMA YA MADIWANI BUKOBA KUJULIKANA KESHO

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana kesho tarehe 23.8.2013 ikifuatiwa na Halmashauri Kuu keshokutwa asubuhi  ambapo itakuwa kwa siku mbili. Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa  kujadili maoni ya wana CCM juu ya Rasimu ya Katiba, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala ya Utumishi.
Alisema siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24, kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.

No comments:

Post a Comment