aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 25, 2014

NANDO ATANGAZA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA (UNGA)....ASEMA BADO ANATUMIA BANGI KWA HIVI SASA JAPO AMEPUNGUZA KIDOGO


Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za kulevya.
 
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha.
 
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.
 
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pia pressure na watu nilokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi...ni yale maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.
 
Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi.
 
“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku.”
 

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali cha kuvuta bangi  kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.

>>Times Fm