aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, June 15, 2014

MAKUBWA HAYA: LULU MICHAEL AFUNGA NDOA YA SIRI AZIANIKA PICHA ZA NDOA YAKE SOMA HAPA

 
Elizabeth Michael aka Lulu is already taken! Na sasa ni mke halali wa ndoa kwa ndugu yetu….!
Sentensi niliyoiandika hapo juu inaweza kuwa rahisi na ya kweli moja kwa moja kwa kuangalia picha za harusi zilizowekwa na muigizaji wa kike Elizabeth Michael aka Lulu kwenye Instagram akiwa ametupia shela na anapewa pongezi kwa kuamua kufunga ndoa.

Lakini ni vigumu sana kuthibitisha kuwa amefunga ndoa kwa kuwa inawezeakana kabisa kuwa alifunga ndoa kwenye filamu yake mpya inayokuja ila ameamua kushare picha kwenye Instagram kuvuta umakini wa mashabiki wake kuupokea mzigo mpya. 
Lulu amepost picha kadhaa Instagram akiwa na shela na kuonesha hatua anazopiga kwa ajili ya kusubiri ndoa yake na kuandika ‘Abt to be some1's Only’, kwenye post ya picha inayomuonesha kwa nyuma.

Mwisho aliweka picha akiwa tayari kwa ajili ya kuvishwa pete na akaandika, “The I do Part”.
Mashabiki wake walimwagia sifa na hongera lakini wengi walichukua tahadhali kama niliyoichukua mimi kuwa huenda ni filamu yake mpya.

“Kwanini lakini unaturusha roho iv? get serious bas” Aliandika shabiki wake mmoja.
Ni vigumu kutenganisha maisha ya uigizaji na maisha ya kweli kwa kuangalia picha. Tusubiri tuone.