aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, June 23, 2014

MAJAMBAZI YAMUUA MDADA, YATOKOMEA NA MKOBA..HUKU DEREVA WAKIMPIGA RISASI YA KIDOLE GUMBA MAENEO YA UBUNGO-DARAJANI KARIBU NA RIVER SIDE LEO


Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.

Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.

Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio.
...Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.
Mwili wa sista ukiingizwa kwenye gari la polisi.

HALI ya hewa imechafuka kwa wakazi wa eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side baada ya majambazi kumuua Sista wa Parokia ya Makoka-Mwisho aliyefahamika kwa jina moja la Kapuli na kisha kumjeruhi dereva wa gari na kutokomea na mkoba wa marehemu kusikojulikana.
Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu leo mchana wakati sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa lengo la kununua mahitaji muhimu.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.
Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi dereva huyo kidoleni.