aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 25, 2014

MACHANGU NI NOMAA...CHECK HAPA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wadada wa mjini waliodaiwa kuwa machangu walimpa wakati mgumu, staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ baada ya kumvamia jukwaani na kumfanyia mambo ya hovyo. 
Tukio hilo lililoshobokewa na wanaume wakware, lilitokea wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Meeda, Sinza – Mori, Dar ambapo mkali huyo aliye Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ alikuwa akiporomosha shoo ya nguvu na kundi lake.
Muziki ulipokolea wadada hao waliokuwa wamevalia nguo saresare walikwenda jukwaani na kuanza kucheza kabla ya baadaye kuanza kujiachia kihasarahasara.
Madada hao wakicheza kwa furaha.
“Mh! Hawa wadada vipi? Mbona wanaleta mambo ya Kanga Moko hapa? Cheza gani ile ya aibu namna ile...hawa lazima ni machangu. Wamekosa wateja sasa wamekuja kumtega Choki, maana mambo yale kama siyo machangu utawaitaje?” alisikika dada mmoja akisema ukumbini humo.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwa wanaume wakware ambao kwao ilikuwa faraja kujionea mambo ya chumbani hadharani, kwani walikuwa wakiwashangilia.
Hata hivyo, wakati wadada hao wakiendelea kufanya yao, Choki wa watu hakuwa na la kufanya, zaidi ya kuduwaa na kuwashangaa tu.
Ili kuonyesha kuwa vichwani mwao hamnazo, wadada hao hawakuona haya kuachia maungo yao wazi, hata pale makufuli yalipobaki nje,  walionekana hawana habari kabisa.
Ilifikia mahali, mmoja wao akaenda mbali zaidi baada ya kutaka kuvua nguo, hakupewa nafasi hiyo, mabaunsa walimbeba na kumtoa ili wastaarabu waendelee kuburudika na Wazee wa Kizigo.

No comments:

Post a Comment