aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, June 1, 2014

MASTAA, WANANCHI WAKUSANYIKA HOSPITALI YA KAIRUKI KUUPOKEA MWILI WA TYSON

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me'. 
Mke wa marehemu Tyson, Beatrice Shayo akiwa na simanzi wakati akiusubiri mwili wa mumewe.
Dada wa marehemu Tyson, aitwae Doreen akisubiri mwili wa kaka yake.
Ni majonzi kwa kila mmoja aliyefika kuusubiri mwili wa marehemu Tyson Hospitali ya Kairuki, Mikocheni, Dar.
Msanii wa filamu za Kibongo, Kelvin akitoa hisia zake kwa mwandishi wetu juu ya kifo cha mwongozaji filamu, GeorgeTyson.
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachoruka kwenye runinga ya EATV, Joyce Kiria akilia kwa uchungu.
Mwigizaji Aunt Ezekiel naye alikuwepo kupokea mwili wa Tyson.
Wema Sepetu nae alikuwepo wakati wa kupokea mwili wa Tyson.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akibadilishana mawazo na mmoja wa waombolezaji.
Mlinzi wa mochwari katika Hospitali ya Kairuki akiusubiri mwili wa Tyson.
Mr. Chuz akielezea alivyoupokea msiba wa George Tyson.