aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, June 7, 2014

KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUPIGWA AKITUHUMIWA NI MWIZI JAMBO AMBALO BAADAYE LILIKUJA KUBAINIKA KUWA SIYO MWIZI


Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la sule amenusurika kifo baadaya kupigwa na watu wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni mwizi jamboambalo baadaye lilikuja kubainika kuwa hana hatia yoyote. 
 
Wakizungumza eneo la feri jijini Dar es salaam baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa inasikitisha kuona watu wakijichukulia sheria mikononi bila kuhoji tukio ambapo mara baada ya kipigo ambacho kimemsababishia majeraha makubwa kijana huyo hakuna mtu aliyejitokeza kulalamika kuibiwa wala kujulikana kijana huyo ameiba nini.
Akiongea kwa shida kijana huyo amesema kuwa yeye hakuiba chocho na hajui kwa nini watu walimvamia na kuanza kumpiga
 
Katika hatua nyingine ya kujaribu kunusuru maisha ya kijana huyo baadhi ya wasamalia wema waliamua kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya usalama lakini mara baada ya kumfikisha katika kituo kidogo kilichopo karibu na hapo walikuta kituo hicho kimefungwa na kufuri na hakuna askali yoyote lakina baada ya muda askali polisi mmoja alitokea..

Bonyeza  hapo  chini  kuona  video  ya  tukio  hilo