aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, June 27, 2014

ANGALIA PICHA MAJAMBAZI WAWILI WALIOUAWA JANA

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita. 

Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.

Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi ambacho hakijafahamika na   kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo. 

Aidha majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.

Jeshi la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.

Wakiwa wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza  kuwashambulia askari kwa risasi lakini dereva wa porisi alimfuta moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki hapo hapo.

 Baada ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa kupelekwa hospitali.

Taharuki hiyo iliyokuwa imeikumba mji wa Geita kwa masaa takribani 3 kabala hawajakamatwa majira ya saa2 baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.

CHEKI HII PICHA YA PROFESSOR JAY AKIWA ENZI ZAKE ZA ZAMANI


Hii  ni  Picha  ya Professor Jay ambayo  kaishare ikimuonyesha yupo na mdogo wake enzi zao za zamani.

MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI WAAGWA JIJINI DAR LEO

Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014
Sista Brigitte Mbaga aliyekuwa na marehemu Cresensia Kapuli eneo la tukio siku alipopigwa risasi akiwa na simanzi.
Mwakilishi wa mama watawa wakuu wa shirika la malkia kutoka Mbeya akilia kwa uchungu.
Jeneza likiwekwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Mbeya kwa maziko.
SIKU YA TUKIO

SISTA Cresensia Kapuli aliyepigwa risasi Jumatatu Juni 23, 2014 maeneo ya Ubungo, River Side na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatimaye ameagwa katika Parokia ya Makoka, Kibangu jijini Dar.
Mwili wa marehemu umeagwa na umati wa watu wa rika zote wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Juni 28, 2014.
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

MAHABUSU WA RUMANDE GEITA LEO WALIPOVUA NGUO KUGOMEA HALI MBAYA YA RUMANDE

MAHABUSU MKOANI GEITA LEO WAMEAMUA KUVUA NGUO,WAKIDAI HAKI ZAO,UAMUZI HUO ULIIBUA TAFRANI MPAKA JESHI LA POLISI KUINGILIA KATI.


ANGALIA PICHA MBINU MPYA YA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA YABAINIKA MKOANI KILIMANJARO

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akitoa dawa za kulevya katika mikoba ya kike ambayo imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.




Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akiwaonesha waandishi wa habari(hawako pichani)moja ya mikoba iliyotumika kufichia dawa za kulevya kwa ustadi mkubwa.
Dawa za Kulevya ambazo hazijafahamika ni aina gani zikiwa katika mifuko maalumu.

Wednesday, June 25, 2014

NANDO ATANGAZA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA (UNGA)....ASEMA BADO ANATUMIA BANGI KWA HIVI SASA JAPO AMEPUNGUZA KIDOGO


Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za kulevya.
 
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha.
 
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.
 
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pia pressure na watu nilokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi...ni yale maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.
 
Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi.
 
“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku.”
 

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali cha kuvuta bangi  kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.

>>Times Fm

MWANACHUO WA CBE AWEKA PICHA ZA UTATA MTANDAONI KUTAFUTA MABWANA,CHEKI HAPA

Hizi ni baadhi ya picha za wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Dodoma ambazo zipo mtaani zimevuja baada ya kuchanganya mabwana mapedeshee wa zaidi ya mmoja katika sehemu tofauti tofauti kati kati ya mji wa Dodoma,
 
Pia chanzo chetu cha habari kilishindwa kuwataja hao mapedeshe kwa kuwa watu maarufu sana kwa kuhofia usalama wao:tunakishukuru chanzo chetu cha habari kwa kufichua maovu kwani tunapiga vita maovu yanayofanywa na wanafunzi wa vyuo vyote pamoja na jamii nzima hatutasita kufichua

PICHA ZA UCHI ZA MAMA WEMA SEPETU ZASAMBAZWAA...WEMA ALIPOZIONA AZIMIA, APEPEWA NA AUNT EZEKIEL NUSU SAA NZIMA!!!

Diva katika tasnia ya filamu Bongo Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.

Katika jambo ambalo limeuumiza moyo wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ tangu awe staa, ni ishu iliyotokea wikiendi iliyopita baada ya mtu asiyejulikana kutengeneza picha chafu ya mama mzazi wa mrembo huyo, Mariam Sepetu na kisha kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho kilimshtusha na kujikuta akipoteza fahamu 
Akizungumza mmoja wa marafiki zake wa karibu ambaye aliomba chondechonde asitajwe , mara ya mwisho kuona chozi la Wema ni siku ya msiba wa marehemu baba yake, mzee Isaac Sepetu lakini hili lilizidi kilio kile kwani ni tukio la udhalilishaji kwa mzazi wake huyo hivyo kuzimia ilikuwa ni lazima kwani yaliyomkuta yanasikitisha.
Chanzo hicho kilidai kwamba, Wema hakutegemea kama ipo siku mama yake atadhalilishwa kiasi hicho hadi kufikia yeye kupoteza fahamu.
“Kiukweli ile picha ilichafua sana hali ya hewa hasa kwa wanaompenda Wema na hata kwa wanaomchukia Wema kwani kila mmoja alikuwa analaani kitendo kile ambacho si cha kiungwana.
“Unajua inafika hatua unatakiwa ufahamu mama wa mwenzio ni mama yako pia halafu usifurahie ubaya anaofanyiwa mama wa mwenzio tutukanane sisi wenyewe na si kuwaingiza wazazi kwenye mambo wasiyojua mbele wala nyuma,” kilidai chanzo hicho.
“Hebu fikiria mama yako mzazi atengenezewe picha ya utupu na jamii iaminishwe kuwa ni yeye wakati si kweli, inauma sana jamani. Utadhani huyo mtu hajazaliwa na mama.”
TIMU DENGUE NA MKAKATI MZITO
Katika kipindi cha vuguvugu la kuchafuana kilichoanza mwanzoni mwa wiki iliyopita, kuna wachangiaji katika mitandao ya kijamii waliojiita kwa jina la Timu Dengue, walionekana kumkandia Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa, timu hiyo ina mkakati mzito wa kumchafua Wema kwa kila namna.
“Wamepanga mkakati mzito, wanadai eti Wema anajisikia. Lakini watu wanasema haiwezekani watu wafanye mambo bila sababu. Sasa hapo wanamhusisha Kajala (Masanja) kwa kuwa ndiye mtu aliye na bifu naye kwa sasa,” kilipasha chanzo hicho na kuongeza:
“Lakini kuna wengine wanabishana, wanadai kuwa inawezekana watu wasio na kazi za kufanya au wenye chuki binafsi na Wema wameamua kutumia mwanya huo kumchafua Wema na familia yake wakiamini lazima Kajala atahusishwa kwa kuwa ana ugomvi naye.”
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Tulipoishuhudia picha hiyo ya utupu na kujiridhisha kuwa siyo ya mama Wema, tulimtafuta Wema kuzungumzia ni kwa jinsi gani alivyoumia baada ya kuona picha ile ambapo majibu yake alionekana bado ana maumivu makali ambayo yalidhihirisha wazi yalikuwa  hayajamuisha moyoni.
“Nimeumia sana mama yangu kudhalilishwa na si mimi tu familia yangu yote kwa jumla, tumeumizwa sana kwa tukio lile lakini mimi nasema namuachia Mungu kwani yeye ndiye anajua ila siyo siri ni tukio ambalo lilinifanya niugue ghafla,” alisema Wema na kuongeza:
“Yaani nilikuwa napewa pole nyingi sana utadhani mimi mgonjwa. Hata wale ambao hawanipendi nao walikuwa wakinipa pole. Naomba serikali itazame upya hili suala hili la watu kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii.”
AUNT EZEKIEL AFANYA KAZI YA ZIADA
Katika ishu hiyo, staa mwenzake wa sinema za Kibongo ambaye kwa sasa ni mashosti, Aunt Ezekiel Grayson alifanya kazi ya ziada kumuokoa Wema na kumfariji asichukue uamuzi mgumu.
Inaelezwa kuwa, Aunt alitumia dakika 29 kumpepea shosti wake huyo ili aweze kurejewa na fahamu, jambo zoezi ambalo lilizaa matunda.
Akizungumza Aunt alisema tukio hilo limemuumiza kila mtu hata wale ambao wanaonekana wako tofauti na Wema lakini kwa hili nao wameumia na kuungana naye kumtetea na kuwakemea waliyofanya kitendo kile.
Mama Wema.
“Nimeumia kwa tukio ambalo limefanywa na kusababisha Wema wangu kulia sana hadi kufikia kuumwa ghafla na kupoteza fahamu. Dah! Binadamu wengine sijui tukoje, lakini hamtaweza kufanikisha kwa sababu Wema ana watu wengi wanaompenda kuliko wanaomchukia,” alisema Aunt.
KAJALA SASA
Tulimtafuta Kajala kupitia simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma za  kuhusishwa na picha hiyo lakini simu yake ilikuwa ikikatika kila ilipopigwa.
Baadaye ilijulikana kuwa, aliamua kuifunga kwa muda (inawezekana alikuwa sehemu inayohitaji utulivu).
Baadaye akatumiwa ujumbe uliosomeka: “Habari. Una taarifa ya picha chafu ya kutengenezwa ya mama Wema iliyosambazwa mitandaoni? Lakini unatajwa kuhusika kwa sababu una bifu na Wema, unasemaje?”
 Kajala hakujibu meseji hiyo wala kupiga simu 
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Jitihada za kuzungumza na mama Wema juu ya sakata hilo ziligonga mwamba kwani simu yake iliita bila kupokelewa.
Msanii Kajala Masanja aliyetajwa katika sakata hilo.
SERIKALI NAYO
Timu yetu ilijaribu kufanya mawasiliano na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba bila mafanikio, kwani simu yake haikupatikana.
Hata hivyo, wananchi wametoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaoni.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, kuliibuka picha chafu katika mitandao ya kijamii za waheshimiwa wabunge, kabla ya baadaye wabunge kulaan ambazo mpaka sasa hazijulikana kuwa zilikuwa halisi au za kutengen
TAHADHARI
Kumekuwa na wingu la kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa hivyo ni vyema kila mtu akachukua taadhari na mamlaka husika ilishughulikie.
source:paparaziwetu

MACHANGU NI NOMAA...CHECK HAPA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wadada wa mjini waliodaiwa kuwa machangu walimpa wakati mgumu, staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ baada ya kumvamia jukwaani na kumfanyia mambo ya hovyo. 
Tukio hilo lililoshobokewa na wanaume wakware, lilitokea wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Meeda, Sinza – Mori, Dar ambapo mkali huyo aliye Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ alikuwa akiporomosha shoo ya nguvu na kundi lake.
Muziki ulipokolea wadada hao waliokuwa wamevalia nguo saresare walikwenda jukwaani na kuanza kucheza kabla ya baadaye kuanza kujiachia kihasarahasara.
Madada hao wakicheza kwa furaha.
“Mh! Hawa wadada vipi? Mbona wanaleta mambo ya Kanga Moko hapa? Cheza gani ile ya aibu namna ile...hawa lazima ni machangu. Wamekosa wateja sasa wamekuja kumtega Choki, maana mambo yale kama siyo machangu utawaitaje?” alisikika dada mmoja akisema ukumbini humo.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwa wanaume wakware ambao kwao ilikuwa faraja kujionea mambo ya chumbani hadharani, kwani walikuwa wakiwashangilia.
Hata hivyo, wakati wadada hao wakiendelea kufanya yao, Choki wa watu hakuwa na la kufanya, zaidi ya kuduwaa na kuwashangaa tu.
Ili kuonyesha kuwa vichwani mwao hamnazo, wadada hao hawakuona haya kuachia maungo yao wazi, hata pale makufuli yalipobaki nje,  walionekana hawana habari kabisa.
Ilifikia mahali, mmoja wao akaenda mbali zaidi baada ya kutaka kuvua nguo, hakupewa nafasi hiyo, mabaunsa walimbeba na kumtoa ili wastaarabu waendelee kuburudika na Wazee wa Kizigo.

WAKUBWA TU..MWANAMUZIKI CHIPUKIZI WA INJILI APIGA PICHA ZA AIBU KWA AJILI YA KUTAFUTA RIDHIKI....INASIKITISHA SANA ANGALIA MWENYEWE KWA MACHO YAKO..!

  

Hapa inadaiwa ni Guest kwa mujibu wa maelezo yake kwenye mtandao. 

Tangu mtandao huu uwe mstari wa mbela kupiga vita tabia mbaya kwa wasichana mbalimbali kuacha kupiga picha za aibu kwenye jamii na kutoa picha kadhaa kwenye mtanA
Hapa Natasha akiwa na nguo za heshima kwenye jamii.


Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni msichana ambae yuko karibu na Natasha anaeishi maeneoya KAWE jijini Dar alisema kuwa picha hizo zimesambaa mitandao na mtu aliyezisambaza ni yeye mwenyewe ambapo ziko nyingine mbaya zaidi ambazo msichana huyo anaonekana kujipapasa sehemu zake nyeti kwa lengo la kuwatia mshawasha wanaume dhaifu.

 KUMRADHI KWA PICHA HII:Natasha akipiga picha za aibu makusudi ili kumtumia mwanaume yeyote atakaevutiwa nae ili amnunua.

KANISA LAFICHUA SIRI KIFO CHA SISTA

mwili wa marehemu

Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka limefichua siri kuhusu mauaji ya Sista Cresensia Kapuli (50), aliyeuawa na majambazi kwa kupigwa risasi kwamba alifikwa na mauti hayo wakati akitoka benki kuweka fedha za sadaka ziliyopatikana Jumapili iliyopita.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo,Kamisha Suleiman Kova


Mwenyekiti wa Parokia hiyo, John Bosco Komba, aliliambia NIPASHE jana kuwa sista huyo aliuawa baada ya kutoka benki ya CRDB tawi la Mlimani City kuweka fedha za sadaka na makusanyo ya Shule ya Sekondari ya Mwenyeheri Anuarite.

“Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kwamba ameporwa fedha zinaweza zisiwe na uhakika sana kwa sababu alitoka benki kuweka fedha za makusanyo ya sadaka, ndipo akapitia kununua mchele zaidi ya kilo mbili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa hiyo hakuwa na fedha nyingi kama inavyoelezwa na watu,” alisema.

Komba alisema Sista Kapuli mbali na kuwa mhasibu wa shule,pia alikuwa mhasibu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka na kwamba siku ya tukio alikuwa na mwenzake Sista Brigitha ambaye ni Mwalimu Mkuu msaidi wa Shule ya Sekondari Mwenyeheri inayomilikiwa na kanisa hilo.

Alisema walipofika katika duka walilokwenda kununua mchele Sista Brigitha ndiye aliyetelemka kwenye gari kwenda kununua na ndipo ghafla majambazi wawili waliokuwa katika pikipiki walitokea na kupiga risasi moja iliyovunja kioo cha gari ambayo ilimjeruhi dereva wa gari hilo, Mark Patrick Mwarabu. 

Aliongeza kuwa majambazi hao walidhani kuwa mkoba aliokuwa nao ulikuwa na fedha nyingi walimpiga risasi mbili Sista Kapuli eneo la titi upande wa kushoto na kufa papo hapo.

Alisema madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wataufanyia uchunguzi mwili wa Sista Kapuli leo kwa ajili ya kumuondoa risasi kabla ya taratibu za kuusafirisha mwili huo kuupeleka kwao katika kijiji cha Mkulwe wilayani Mbozi, mkoani Mbeya.

Alisema baada ya taratibu za uchunguzi wa mwili huo kufanyika, kesho mwili utapelekwa katika Kanisa la Makoka kwa ajili ya misa na kuuaga na safari ya kuusafirisha kwenda kijijini kwao wilaya ya Mbozi itaanza huku akisema kifo hicho kimewasikitisha.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kuanza kwa msako ili kuwabaini na kuwakamata majambazi waliohusika katika tukio hilo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamisha Suleiman Kova, alisema jana kuwa Jeshi lake limeandaa operesheni maalumu itakayohusisha vikosi tofauti ili kuwatia mbaroni wahalifu hao, ambao alisema walipora Sh. milioni 20

source:nipashe

Monday, June 23, 2014

WATOTO KUANZIA UMRI WA MIAKA 10 WATAANZA KUPEWA KONDOMU BURE NA DAWA ZA KUPANGA UZAZI


Kuna sheria mpya inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Senet ambayo sheria hiyo itawaruhusu watoto kuanzia miaka 10 kupewa mipira ya kondomu na dawa za kupanga uzazi. 


Sheria ya afya ya uzazi ya  mwaka  2014 ambayo tayari ipo mbele ya Senet, inasema kuwa elimu kwa watoto kuhusu afya ya uzazi na ngono wapewe watoto pengine hata bila ya wazazi kutoa idhini.
 
Sheria hiyo imewasilishwa na Seneta mteule Bi.Judith Sijeny anayesema kwenye pendekezo la mswada huo kuwa watoto wanaovunja ungo wapewe nafasi yakutosha kupata habari kamilifu kuhusu elimu ya ngono na huduma za kisiri ikiwa ni pamoja na habari za kutosha na orodha ya dawa za kupanga uzazi na habari kuhusu ujauzito na uzazi wa mpango.


Muswada huo unaashiria kwamba wanaovunja ungo ni walio kati ya umri wa miaka 10 na 17 ambao ni wanafunzi kati ya darasa la tano na kidato cha tatu.

KICHANGA CHATUPWA KWENYE DAMPO LA TAKA


Kichanga kinachokadilwa kuwa na umri wa miezi kati ya 6-7 kimekutwa kimetupwa kwenye dambo karibu na mahakama ya mwanzo mkabala na ofisi za manispaa ya Iringa, mkoani Iringa na mwanamke mmoja ambaye hakufahamika mara moja leo.


Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema wanamtafuta mwanamke aliyefanya kitendo hicho ili sheria iweze kuchukua mkondo wake pamoja na kukomesha vitendo hivyo mara moja .