aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 1, 2013

wakazi wa mtwara waipokea kwa shangwe semina ya fursa kwa vijana leo.




Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume akizungumza 
mapema leo kwenye semina ya FURSA kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa
 Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa 
NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi
 Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye
 pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini
 mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na
 Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na
 wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo
 wasanii wa
 muziki wa kizazi kipya.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini
 yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo 
ndani ya ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani 
Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),
Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi 
kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo
 fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya
 kuzifanyia
 kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha.

Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya 
Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste
 Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,
Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF 
mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari
 imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.






Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina 
hiyo ya Fursa kwa vijana

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpo ambaye pia ni mwanachama wa NSSF,akizungumza fursa mbalimbali alizozipata ndani ya shirika hilo la NSSF,mbele ya 
wakati lukuki wa mji wa Mtwara waliojitokeza kushiriki semina hiyo,iliyokuwa na mafanikio makubwa.


Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semini hiyo 





Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.Katika semini hiyo vijana wemejitokeza kwa wingi.

Msanii wa Kughani mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na Wana wa Mtwara 
kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huu,kwenye semina ya Fursa
 kwa Vijana iliyofanyika leo mkoani humu.

Baadhi ya Waendesha Bodaboda walipata wasaa wa kuacha kazi zao na kushiriki 
semina ya Fursa kwa Vijana.

Baadhi ya vijana wakiwa nje wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea ukumbini 
Picha na Michuzi Jr

No comments:

Post a Comment