aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 29, 2013

TASWIRA ZA SHEREHE YA MWAKA MMOJA WA THE LEGEND IS BACK NDANI YA ISUMBA LOUNGE

Keki ya sherehe hiyo.
John Diliinga maarufu kama DJ JD akiwa kazini.
Wadau wakijiachia katika sherehe hizo ndani ya Isumba Lounge.
DJ Fast Eddy akifanya vitu vyake.
Wadau katika pozi.
JANA palikuwa hapakaliki ndani ya kiwanja wa Isumba Lounge zamani kikijulikana kama Jolly Club ambapo DJ mkongwe nchini John Diliinga maarufu kama DJ JD alikuwa akifanya kumbukumu ya mwaka mmoja katika fani yake hiyo.
Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na vijana wengi wa kitambo ilifana vilivyo ambapo madansa wa zamani wa kucheza muziki Athuman Digadiga na mwenzake Maneno Ngedere walikumbushia enzi zao za kucheza aina mbalimbali ya muziki.
Mbali na wakali hao pia wakongwe wa kucheza muziki wa Chacha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wakati huo Muddy Jazz B  na mkali mwenzake Sunday Boy walikumbushia makali yao na kushangiliwa kwa nguvu na wadau walioibuka katika shoo hiyo.
Awali katika 'event' hiyo iliyonogeshwa na muziki mbalimbali wa miaka ya nyuma mbali na DJ JD pia swahiba wake DJ Fast Eddy walionogesha usiku huo kwa kushusha burudani ya nguvu iliyowafanya wadau kutopata muda wa kukaa katika viti vyao.

No comments:

Post a Comment