aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 26, 2013

MTOTO AAMUA KUNYWA SUMU YA PANYA BAADA YA KUONA ANADHULUMIWA MALI ZA BABA YAKE..!!


MTOTO Alan Kewa (12) mkazi wa Keko Mwanga anadaiwa kunywa sumu ya panya kwa kile kilichodaiwa alitaka kujiua baada ya kuona anadhulumiwa mali za marehemu baba yake.
Kamanda wa Polisi wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema sababu nyingine ya mtoto huyo kutaka kujiua ni pamoja na kutolipiwa ada ya shule na shangazi yake aliyefahamika kwa jina moja la Barched.
Kwa mujibu wa Kamanda, mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya polisi ya Barracks kwa matibabu zaidi na juhudi za kumtafuta shangazi yake zinaendelea.

No comments:

Post a Comment