aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 26, 2013

DAWASA SASA KUPANDISHA BEI YA MAJI MARADUFU......!!




MAMLAKA ya Maji safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASA) imeomba kuongeza bei ya maji kwa Sh 12 kwa lita.
Akizungumza kwenye taftishi kuhusu maombi ya kurekebisha bei za maji, Ofisa Mipango wa DAWASA, Anthony Masawe alisema ongezeko hilo ni kutoka Sh 20 kwa lita 20 za maji hadi kufikia Sh 32 kwa ujazo huo.
Alisema wameomba bei ya rejareja kuongezeka kutoka Sh 1,077 hadi Sh 1,627 kwa mita za ujazo za majisafi, huku bei ya majitaka ikiongezeka kutoka Sh 275 hadi Sh 302 kwa mita za ujazo wakati bei ya jumla kuwa Sh 856.
Masawe alisema sababu za kuomba ongezeko hilo ni katika kuwapa uwezo wa kutekeleza mpango wake wa kibiashara wa miaka mitatu wa kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2016 ambao una mikakati mbalimbali ya utekelezaji, ikiwemo uboreshaji wa huduma za majisafi na maji taka jijini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik aliwataka DAWASA kuhakikisha wanatoa huduma stahiki na kwa wakati kwa wananchi na kutoa ankara ya maji iliyo halisi, ili kuondoa malalamiko miongoni mwa jamii.
Sadik pia ameitaka EWURA kuhakikisha inatoa bei elekezi katika huduma ya maji yanayouzwa katika boza.

No comments:

Post a Comment