aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, July 7, 2014

WANANCHI WAFURAHI KUMUONA RAIS KIKWETE AKIJUMUIKA NAO KWENYE MAONYESHO YA SABA SABA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwamara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya siku ya Jumamosi kutokana na muda. 

Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila mwaka.

Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila mara alisimama na kuwasalimia. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliotembelea maonyesho ya Sabasaba.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta na watoto aliokutana nao Sabasaba.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaaga wananchi mara baada ya kujumuika nao pamoja kwenye Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar. PICHA NA IKULU