aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, July 14, 2014

HALI YA MTOTO DEVOTA ALIYEFUNGIWA UVUNGUNI KWA MIAKA SITA YABADILIKA NA KUHAMISHIWA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO.


Mtoto Devota Malole aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kufuatia mama yake kumtesa kwa kumfungia ndani na kumlaza chini kwa muda wa miaka mitano amehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya afya yake kiafya kubadilika.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema wamelazimika kumuhamishia mtoto huyo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya hali yake kuwa mbaya na uchunguzi wa awali umebaini anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika hospitali ya mkoa wa morogoro waandishi wetu wameshuhudia madaktari wakifanya kila juhudi za vipimo na matibabu.

Wasamaria wema wamejitokeza katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia hali mtoto Devota ambapo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood amewataka maafisa ustawi wa jamii kuacha kulala na badala yake watekeleze wajibu wao ipasavyo kuwasaidia watoto wanaoteseka .


Nae mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya Alsaidi Omari Alsaidy ameahidi kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata kama italazimika kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.

No comments:

Post a Comment