aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, July 21, 2014

KANISA LAFUNGWA BAADA YA MCHUNGAJI WA KANISA HILO KUFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIJIANDAA KUNGONOKA NAYE NDANI YA KANISA..


Mwanzoni  mwa Mwezi  July  2014, Mchungaji Michael Semeni wa Kanisa la Living Word Ministry lililopo Ukonga- Majumba Sita jijini Dar es Salaam  alifumaniwa  live  akijiandaa  kuvunja  amri  ya  sita  na  muumini  wake  ambaye  ni  mke  wa  mtu  ndani  ya  ofisi  yake.

Mchungaji Semeni alinaswa akiwa na mwanamke huyo aitwaye Erizabert Kisanda, mkazi wa jijini Mwanza ambaye alifika Dar kuonana naye kwa ajiliya kumwombea maombi maalum ya kiroho ‘deliverance’ kutokana na matatizo ya mke huyo kushika mimba na kutoka kila wakati.

“Huyu mwanamke alikuja Dar kwa mchungaji kwa lengo la kuombewa apate mtoto. Alikuwa na tatizo la uzazi kwani kila alipopata ujauzito, akikaribia kujifungua tu mimba inaharibika.
 

“Kutokana na tatizo hilo, ndipo akashauriwa akamwone mchungaji huyo ndipo akafunga safari kwenda kumuona na kumweleza tatizo lake, mchungaji akamwambia ni tatizo dogo sana kwake.”  Anasimulia  shuhuda  wa  mkasa  huo.

Ilizidi kudaiwa  kwamba, ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya tukio.

Siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kuombewa ambapo mchungaji  huyo alizama kiroho zaidi kwa muda wa saa mbili.

“Baada ya kumaliza maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo akamchombeza kwa kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,”chanzo kilisema.
  
Habari zaidi zinadai  kuwa wakiwa chumbani sasa, mke hana nguo, mchungaji akiwa ndani ya kipensi tu, mwanaume aliyedaiwa ni mume na dada yake walitokea kusikojulikana na kuwavaa, hali  iliyosababisha  tafrani  kubwa.

Kuhusu kilichotokea baadaye  baada ya  fumanizi  hilo  ni kwamba kanisa hilo limefungwa. Mara baada ya waumini  wake kuona fumanizi  la  baba mchungaji huyo  walisusa kwenda kanisani hapo.

Habari zilizonaswa kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja  zilidai kuwa baba mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo.
  
“Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa mtumishi wa Mungu. Baada fumanizi  lile, baba mchungaji  hajaonekana tena na kanisa limefungwa,” alisema mmoja wa waumini hao

No comments:

Post a Comment