aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 2, 2014

SHETTA APATA DEAL DSTV, NI BAADA YA KUACHIA VIDEO YA KEREWA, AMSHUKURU DIAMOND KUMPA MWONGOZO KATIKA USHINDANI WA SOKO LA MUZIKI AFRIKA


Rapper Shetta amedai kuwa baada ya kutoka kwa video yake mpya ya Kerewa tayari ameshaanza kupata deal za pesa ambapo DSTV wameshaonyesha nia ya kufanya kazi na msanii huyo.


kerewa

Akizungumza Shetta amesema kuwa tayari wapo kwenye mazungumzo na no na DSTV na hivi karibuni kila kitu kitakuwa wazi.

“Wakati Diamond ananiambia ‘weka hela Shetta usiogope kuweka hela kutangaza muziki wako kuwa tofauti na wanamuziki wengine, fanya muziki wako kufika mbali’, akimaanisha soko la Afrika nikaona kama ananitania hivi, almost alikuwa ananiambia kama milioni 20 hivi ukiitoa ile hela ambayo Godfather ninamlipa, nikaona mbona ni pesa nyingi sana.

 Lakini nimejaribu kudhubutu, hiki unachokiona ni king’amuzi cha DSTV ni kama fursa ambayo nimekutana nayo ni deal ambayo ikiwa rasmi zaidi watu watagundua nini ambacho kimetokea, lakini mpaka hapa tulipofikia ni kama nusu yake au robo tatu yake. 

Godfather aliniconnect na watu wa DSTV, tukafanya makubalianao na makaratasi yapo. 

Video yangu imepata rotation kubwa sana, katika station zote ambazo zinaonekana DSTV, na wamenifollow kwenye akaunti zangu, wananitangazia vitu vyangu kwenye akaunti zao, kwahiyo hiyo ni deal kwa upande wangu.

 Thanks to Diamond, thanks to Tale na watu wote ambao wamenisupport. Kwahiyo sijutii kwa pesa niliyoweka,” alisema.

CHECK VIDEO YA KEREWA >>HAPA<<