aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 3, 2014

JERRY SLAA AMKIMBIA MKEWE

MEYA wa Ilala, Jerry Slaa ameonyesha kituko cha aina yake kwa kumkiambia mkewe baada ya kuona nyoka akielekezewa upande alipokuwa ameketi. 
Meya wa Ilala, Jerry Slaa ndani ya Ukumbi wa Serena, Posta jijini Dar.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Serena, Posta jijini Dar, ambapo Slaa alikuwa amealikwa kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Watu ndipo alipoambatana na mkewe huyo.
Jerry Slaa akiwa na mkewe usiku huo wa tuzo za watu.
Akiwa kwenye hafla hiyo, ghafla mheshimiwa alijikuta akitimua mbio huku akimuacha mkewe akiwa ameketi kwenye kiti chake baada ya kikundi cha ngoma za asili kuanza kutumbuiza na mmoja wao akichezea nyoka huku akielekea mahali alipokuwa ameketi Slaa na mkewe.
Hata hivyo, nyoka huyo alirudishwa na baadaye Slaa akarejea alipokuwa ameketi awali.