aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 22, 2014

MWANAMKE AMWAGIA MUMEWE MAJI YA MOTO SEHEMU ZA SIRI KISA.. SOMA ZAIDI HAPA !!!


MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma Said mkazi wa Kitunda, Ilala jijini Dar es Salaam anashikiliwa na Polisi baada ya kummwagia maji ya moto mumewe sehemu za siri na tumboni kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi, tukio lililotokea Julai 16 mwaka huu, huko Kitunda.
Majeruhi Adam Rashid akiwa amelazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam kwa majeraha ya maji ya moto.
Chanzo chetu cha habari kililiambia paparazi kuwa tukio hilo lilitokea saa 12.30 jioni baada ya mwanaume huyo, Adam Rashid ambaye ana wake wawili, kwenda katika nyumba anayoishi mke mkubwa akiwa ameandamana na mke mdogo, kwa lengo la kupata maji ya kuoga na kubadili nguo, akitokea kituo kidogo cha Polisi Stakishari, ambako aliwekewa dhamana kwa shauri lililokuwa likimkabili.
Inadaiwa kuwa baada ya kuwekewa dhamana hiyo, Adam na mkewe mdogo, Aisha Juma, waliamua kwenda nyumba anayoishi mke mkubwa, ambayo inamilikiwa na mwanaume huyo,  kwa ajili ya kuoga na kubadili nguo, wakiamini kuwa kusingekuwa na matatizo yoyote kwa vile wanawake wote wawili anaishi nao kihalali na wanafahamiana.
Inasemekana kuwa baada ya kufika nyumbani hapo, Adam alimtaka mwanaye kumwandalia maji ya kuoga na akimaliza apewe bukta, ili aweze kuondoka na mke mdogo kuelekea wanakoishi, lakini wakati hayo yakifanyika, bi mkubwa alianza kutoa maneno machafu ya kejeli, yaliyoonyesha wazi kuwa alikuwa na wivu wa kimapenzi.
Majeraha ya maji ya moto aliyopata Bw. Adam Rashid.
Baada ya mwanaume huyo kumaliza kuoga na kutoka nje, inadaiwa mkewe mkubwa alijitokeza akiwa amebeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto, yanayodaiwa kuwa yalitakiwa kutumika kwa ajili ya kupikia wali na kumwagia tumboni na sehemu za siri, huku akiendelea kumtolea maneno ya kashfa.
MAJERUHI ALONGA
Akiwa amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, majeruhi  Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu alienda  nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake zake.
“Baada ya kunimwagia maji, mke wangu mdogo alilia sana kwa uchungu, majirani wakanichukua na kunipeleka Polisi ambako tulimkuta bi mkubwa akiwa anaandikisha maelezo kuwa mimi nimempiga, kuona vile askari walimgeuzia kibao na kumwingiza ndani kwa ajili ya mahojiano zaidi.”
Adam Rashid akifunguka kuhusu mkasa uliompata kwa waandishi wetu.
MKE MDOGO NAE
“Ndugu  mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi  kwa  mke  mkubwa bila wasiwasi  maana  na  mimi pale  ni  kwangu  kwa  sababu  nyumba  ya  mume  wangu  halali, lakini tulipofika tuliambulia  maneno  machafu na kejeli.
Mke mkubwa alihoji kwa jeuri kitu gani tulichokifuata pale, mume wangu alikuwa akimjibu kuwa hapa nipo kwangu na huyu  niliyekuja naye ni mke wangu halali, mbona unanifanyia mambo ambayo  siyaelewi, yule hakuelewa, aliendelea tu na maneno yake machafu.”
KAMANDA WA POLISI

Kamanda wa polisi  mkoa wa kipolisi Ilala, SACP 

Marieth Minagi amethibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo

 na kusema mtuhumiwa  huyo anashililiwa katika 

kituo  cha polisi Wilaya ya kipolisi Ukonga na

 amefunguliwa jalada na kupewa namba 

RB/STK/9438/2014 KUJERUHI 

na uchunguzi unaendelea.....