Mamlaka ya Marekani inayoshughulikia usalama katika safari, haitoruhusu simu za mkononi ama vifaa vingine vya elektroniki za abiria wanaoenda Marekani kwa ndege kutoka katika viwanja vya ndege vya nchini mbalimbali duniani kama vifaa hivyo vitakuwa havina chaji.
Hatua hiyo ya mamlaka hiyo ya TSA ilitangazwa wiki iliyopita kuboresha usalama kufuatia kuwepo taarifa kuwa kundi la Al Qaida nchini Yemen na kundi la kiislamu la Nusra Front lenye uhusiano na al Qaeda nchini Syria, yamepanga kulipua ndege.
Kutokana na kuwepo na hofu katika baadhi ya viwanja vya ndege duniani, askari wa usalama wanaweza kuwataka abiria kuwasha simu zao katika vituo vya ukaguzi na kama zikiwa hazina chaji hazitaruhusiwa kuingia kwenye ndege.
Wataalam wa masuala hayo wanadai kuwa komputa za laptop ni miongoni mwa vitu walinzi wanaweza kuwataka abiria waviwashe.
Maafisa wa Marekani wanahofia kuwa simu za mkononi, tablet, laptop ama vifaa vingine vya elektoniki vinaweza kutumika kama bomu.
Maafisa hao wamezitaja simu zitakazokuwa zikikaguliwa ni iPhones naSamsung za abiria wanaotoka kwa ndege kutoka Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika.
No comments:
Post a Comment