aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

RAMADHANI YAMALIZA BIFU LA WEMA SEPETU NA PENNYStaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 
Wakizungumza, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”
 
Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”


Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.