aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 13, 2014

MCHEPUKO: STAA WA FILAMU ANASWA USIKU NA MKE WA MTU!..PAPARAZI CHUPUCHUPU AGONGWE STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, StanleyMsungu amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.
Staa wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu
Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonitaamefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.
...akijificha kukwepa Kamera.
“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.
Mke wa mtu anayedaiwa kuchepuka na Stanley Msungu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, paparazi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.
“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu akijitetea huku Bonita akiomba kamera ya paparazi iishe chaji ili zoezi la kupiga picha lisiendelee kabla ya kuondoka eneo hilo kwa spidi na kutaka kumgonga paparazi.