aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 5, 2014

DUDUBAYA ASAKWA NA POLISI


MKONGWE wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ anasakwa na polisi kwa RB namba OB/RB/11650/2014 KUTISHIA KUUA mganga wa jadi Mery Kapalisya ambaye inadaiwa alikuwa akiishi naye kama mkewe.
Mkongwe wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya'.
Akisimulia mkasa mzima, Mery alisema Dudubaya alitishia kumuuamara baada ya kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja maeneo ya Tandale, jijini Dar.
“Mimi na Dudu (Dudubaya) tulikutana baada ya kukutanishwa na Mabovu (msanii) ndipo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya kuniomba niwe naye na kunieleza matatizo yake.
“Kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa tukilala katika baa yangu  nyumbani kwa akina Mabovu.
“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya  alianza kunibembeleza kwamba baa ile tuipe jina la Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia lakini nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili ambazo zitamaanisha na mimi nahusika, tukakubaliana,” alisema Mery na kuongeza:
Mganga wa jadi Mery Kapalisya ambaye amedaiwa kuishi na 'Dudubaya' kama mke wake.
“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo yakaanza taratibu kwani walijaa wasanii wa kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya mpaka wateja wote wakaondoka wale waliokuwa wanajiheshimu.”
Mery alisema alikuwa akimuonya Dudubaya juu ya tabia za kumsaliti na kulala na wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa amesafiri kwenda kwenye mambo ya kitabibu lakini alikuwa hasikii.
“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia maneno mazito sana ambayo siwezi kusimulia kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,” alisema Mery alipokuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Wakati Mery alipokuwa kituoni hapo, polisi walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo ya polisi kisha akakata simu na alipopigiwa tena, hakupokea.