aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 29, 2014

SASA NI ETO’O MAHAKAMANI: SABABU NI KUSAMBAZA PICHA ZA UTUPU ZA MPENZI WAKE WA ZAMANI

pix_1402578975e131615_1Eto’o anaweza kuuhesabu 2014 kama mwaka mbaya kwake baada ya timu yake ya taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia hana Club ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, kama hiyo haitoshi kwa sasa kilichombele yake ni kesi nzito Mahakamani. 
Kesi hizo za udhalilishaji ni kutokana na kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu na udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba wake wa zamani Hélène Nathalie Koah.
Screen Shot 2014-07-28 at 3.01.52 AMMapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo huku hili likiwa limetokea siku chache baada ya kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook ambazo mhudumu huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.
Eto’o amekanusha kuhusika na hilo na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
Screen Shot 2014-07-28 at 2.59.36 AMWakati hayo yakiendelea, kaa ukifahamu kwamba Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye ugomvi mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o baada ya kuwachanganya kimapenzi.

Monday, July 28, 2014

LAANA: WACHECK HAWA WAKIJIACHIA JUKWAANI... NISHEEDAAAH

JAMANI HII NI LAANA, ETI HUYU MSICHANA AFANYA ULE UPUUZI WAKUMTUMIA MPENZI WAKE PICHA ZA UCHI. ONA SASA ZIMEVUJA!

2go lover

Dada zetu bana sijui wataacha lini huu mchezo wakuweka picha mbaya kwenye simu zao.Mnadiliki hata kuwatumia wapenzi wenu picha za uchi bila uwoga duuh! Kila muda mnaona matukio mtandaoni wenzenu wanavyoaibika lakini hamkomi. 

Sasa ona naye huyu aliyemtumia mpenzi wake picha za uchi kwenye mtandao wa 2GO.
Jamani ifikie muda mbadilike, sasa tutaona nyeti zenu hadi lini? Tumechoka sasa, mbona ni shida?

MKAZI WA YOMBO KILAKALA AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKE

MKAZI wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, Charles Swai (48), amekutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Englibert Kiondo, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:00 mchana, ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kitandani na haukuwa na jeraha lolote.

Kiondo alisema kifo hicho kiligundulika baada ya Swai kutofungua mlango wa chumba chake tangu alipofunga Julai 23 saa 2 usiku, ndipo majirani walipochungulia dirishani na kumuona akiwa amelala na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Chang’ombe.Alisema askari walifika eneo hilo na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki dunia. Chanzo cha kifo hakijafahamika na mwili umehifadhiwa hospitali ya Temeke. Upelelezi unaendelea.
 
Katika tukio jingine, dereva aliyefahamika kwa jina la Felix Mgoba (25) mkazi wa Wazo, amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na Fuso. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi (ACP), Camillius Wambura, alisema lilitokea juzi saa 5:20 asubuhi huko barabara ya Bagamoyo eneo la Boko Msikitini.

PICHA NA TAARIFA KAMILI ZA AJALI ALIYOPATA BAHATI BUKUKU

Gari waliyokuwemo Bukuku na wenzake.

Usiku , muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma. paparazi ilikuripoti taarifa za awali, na hapa tunakuletea picha kamili na taarifa rasmi ya jeshi la polisi mkoani Dodoma.

Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na kushindwa kugeuka wala kuinuka - akiwa amelazwa. Tayari ndugu na marafiki walishafika kutoka Dar es Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita kuwajulia hali na kuwafariji.

Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranchya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.

Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

Frank amesafishwa kichwa na anaendelea vema. Muujiza wake ni kwamba nguo aliyokuwa amevaa ilichanwa na vioo, lakini yeye mwenyewe hajachubuka kutokana na vioo hivyo.

Picha hizi zilipigwa na Alpha, ambaye alitoka bila kuwa na majeraha kwenye ajali hiyo, wakati dereva, Eddy (Edson Mwakabungu) yeye ameripotiwa kuwa mguu umevimba, kiasi cha kulazimika kutoa jeans aliyokuwa amevaa.

WANAFUNZI WATANO WALAWITIWA KWA MPIGO NA MWENZAO! ABATIZWA JINA NA KUITWA BABU SEYA

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la sita kwa tuhuma nzito ya kuwalawiti wenzake watano kwa mpigo.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri katika Mtaa wa Twanga Pepeta Kijiji cha Fulwe-Dindili Kata ya Mikese Wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani hapa ambapo dogo huyo alidaiwa kufanya tukio hilo ambalo ni gumzo kwa sasa huku raia wenye hasira kali wakitishia kumshushia kipigo denti huyo waliyempa jina la Babu Seya endapo ataachiwa na jeshi la polisi.
 
Mwanahabari wetu alifunga safari hadi kijijini hapo ambapo baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai kwamba dogo huyo alikuwa akiwalawiti wenzake kwa kigezo cha kuwapanga kwenye mechi za mpira wa matambara.
 
lli kupata undani wa tukio hilo, mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kukuta tayari jeshi la polisi lilifika limeshamkamata. 
 
Mjumbe wa serikali ya mtaa huo wa Twanga Pepeta Kitwana Tupa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri sheria ichukue mkondo wake baada ya kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Poul.

Saturday, July 26, 2014

ALI KIBA NA DIAMOND BIFU LAO SASA LAFIKIA PABAYA

Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa). 

Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:
“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema mimi ndiyo nilimfuta.
Staa wa muziki Bongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti kila msanii waTanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.
“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye alitengeneza ule wimbo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu'
“Sikuwahi kwenda studio na Diamond, sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).
Nikamwambia itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo wake, shahidi prodyuza wangu KGT.
“Kutoka hapo nikaona hakuna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri. “Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.
“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” Baada ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu.”
Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe,Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo bado ni mbichi. Tusubiri mwisho WAKE!

MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI:MADAI NI FUMANIZI,KAMANDA WA MKOA ASHTUKA...YASEMEKANA APELEKWA HOSPITALI KINYEMELA...MPAKA LEO POLISI HAWANA TAARIFA KUHUSU TUKIO HILI

NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kichwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa. 

Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani.
Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.
TAARIFA FUPI
Kwenye mitandao ya kijamii, picha hizo ziliambatana na maelezo mafupi sana kwa chini yakisomeka hivi:
“Baada ya madoctor (madaktari) wa Bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliyefumaniwa huko Mwanza hatimaye wamefanikiwa kumtoa shoka kichwani na hali yake bado mbaya, yuko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) kwa uangalizi zaidi. Mke wa mtu sumu!”

Picha ya X-Ray shoka lilivyoingia pichani.
MAZINGIRA YA PICHA
Kwenye baadhi ya picha, mwanaume huyo anaonekana ana nywele ndefu kidogo na mustachi ulionona. Picha nyingine zinamuonea akiwa na kipara nusu kichwa baada ya kunyolewa nywele ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kulitoa shoka hilo lililozama ndani sana.

MAZINGIRA YA HOSPITALI
Baadhi ya watu waliochangia kwenye mitandao ya kijamii walisema tukio hilo lilitokea nje ya Tanzania. Walisema ingekuwa Bongo lazima vyombo vyahabari vingeandika lakini hata hivyo, mazingira ya chumba cha upasuaji alicholazwa mwanaume huyo yalionesha ni Tanzania.

Shoka likiwa limetolewa na madaktari wa upasuaji.
KWA NINI NI TANZANIA?
Ni Tanzania kwa sababu, picha zinamuonesha mwanaume huyo akiwa kwenye kitanda cha chumba cha upasuaji akiwa amefunikwa shuka yenye maandishi yanayosomeka kwa kifupi MSD.
MSD ni kifupi cha maneno Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa). Mbali na kugawa dawa katika hospitali za serikali nchini, pia MSD inatoa mashuka yenye nembo hiyo kwa ajili ya kujifunika wagonjwa mahospitalini.
RPC ASHTUKA
Ili kupata ukweli wa madai hayo kwamba mwanaume huyo alikutwa na mkasa huo mkoani Mwanza na kulazwa katika Hospitali ya Bugando,paparazi liliingia kazini kufuatilia tukio hilo kwa kuzungumza na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime na kumuuliza kama ana ishu hiyo mezani kwake.
“Mh! Hivi nyiye mnajua kama mitandao siku hizi imezua balaa kubwa sana? Hivi tukio kama hilo, mwanaume apigwe shoka mpaka kuzama kichwani, alazwe Bugando Hospital mimi nisijue?
“Hakuna kitu kama hicho.
Hayo ni mambo ya mitandao tu, sijui wametoa wapi? Halafu si umeona hata maelezo hayajitoshelezi? Mimi mkoa wangu upo shwari kabisa mpaka hivi ninavyoongea na wewe,” alisema Afande Fuime kwa sauti iliyoashiria kushtuka.
DAKTARI BUGANDO AONGEA
Ili kuchimba zaidi, paparazi lilimtuma paparazi wake aliye Mwanza,  ambaye alikwenda hadi Hospitali ya Rufaa, Bugando na kuzungumza na daktari mmoja anayefanya kazi kwenye kitengo cha upasuaji ambapo alisema:
“Ni kweli tunapokea watu wenye matukio ya kutisha lakini mwanaume aliyepigwa shoka mpaka likazama kichwani hatujampokea,” alisema daktari huyo akiomba asitajwe jina kwani si msemaji wa hospitali hiyo. 
TUKIO LAHAMISHIWA KAHAMA
Katika hali iliyozidi kuibua maswali, baadhi ya watu waliozungumza na paparazi wa Mwanza walisema wamesikia mwanaume huyo alikumbwa na balaa hilo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
KAHAMA
paparazi alitoa ripoti kwamba, hakuna mwanaume aliyelazwa kwenye hospitali yoyote ya wilayani Kahama wala mkoa huo kwa kupigwa shoka la kichwani.
MASWALI YA MSINGI
Bado jamii imebaki na maswali kadhaa ya kujiuliza. Kwamba, kama ni tukio la Tanzania, hiyo sehemu aliyolazwa mtu huyo hakuna jeshi la polisi? Kwa sababu polisi ndiyo wanahusika na kupewa taarifa za matukio kama hayo na kuyatangaza.

Pili, jamii inauliza kwamba, inawezekana mwanaume huyo baada ya tukio hakupitia au kupitishwa polisi kwa ajili ya kupewa Police Form No. 3 (PF3)?
Kama ni hivyo, hospitali walimpokeaje mtu wa hivyo hasa ikizingatiwa kuwa, hali yake ilionekana ni mbaya kwani hata picha ya X-Ray ilionesha shoka hilo lilizama kiasi cha kama inchi sita kwenda ndani na kubakiza kidogo kutokea upande wa kulia wa kichwa.

SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYOTUPWA DAR: SERIKALI YAIFUNGA HOSPITALI YA IMTU

Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, imefungiwa kwa muda usiojulikana baada ya kugundulika kutokidhi viwango na maadili ya utoaji huduma za hospitali nchini.

Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imechukua jukumu la kuifungia hospitali hiyo baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza na kubaini uwepo wa mapungufu kadhaa.
 
Mapungufu yaliyobainika kuwepo katika hospitali hiyo ni pamoja na kutokuwa na wauguzi wa kutosha, kutokuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo kifaa cha kuchomea taka ngumu, kuchanganya dawa zilizokwisha muda na ambazo hazijaisha muda wake na pia wauguzi kufanya kazi ambazo si za kwao.
 
Akizungumza wakati wa kufunga hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba alisema, hospitali hiyo inastahili kufungiwa kutokana na kutokidhi viwango hivyo.
 
"Baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza tumebaini kuwepo kwa mapungufu haya, kwa hiyo tunaifungia hospitali hii mpaka pale watakaporekebisha," alisema Dk Kamba.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Yassin Mgonda alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo ambayo aliahidi kuyafanyia kazi.
 
Hata hivyo, Profesa Mgonda aliiomba Manispaa na Wizara ya Afya kuangalia adhabu hiyo waliyoitoa .
 
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo wakipata huduma walishtushwa na kusikitishwa na kitendo hicho, lakini walikipongeza na kutaka kuwa endelevu.
 
Mmoja kati ya wagonjwa hao aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kiwalo alisema, ukaguzi huo unatakiwa kuwa endelevu ili kuendelea kufichua madudu yaliyopo katika hospitali mbalimbali nchini.
 
Aidha, Msemaji Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema, endapo hospitali hiyo watatimiza masharti waliyopewa na Mganga Mkuu wa Manispaa wao kama wizara watafanya ukaguzi kuona kama wamekamilisha.
 
Alisema ikiwa watakuwa wamerekebisha kasoro hizo zilizopelekea kufungiwa hospitali hiyo itaruhusiwa kutoa huduma zake kama kawaida.
 
Hospitali hiyo imefungiwa wakati kukiwa kuna sakata linalokihusisha chuo chake, kinachodaiwa kutupa viungo vya binadamu jalalani.
 
Katika sakata hilo lililovuta hisia za watu na kuzua mjadala mitaani, katika vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, watu wanane wakiwemo madaktari wa IMTU, walikamatwa na Polisi kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika katika utupaji viungo vya binadamu jalalani.
 
Serikali wakati ikiendelea kuchunguza tukio hilo ikiwemo kuunda tume nyingine ya watu 15 chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kujiridhisha kabla ya hatua kuchukuliwa iliyopewa siku saba kukamilisha kazi yake, tume hiyo imeundwa kukiwa na tume nyingine iliyoundwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
 
Tume iliyoundwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  imejielekeza kuja na majibu kadhaa,  ikiwa ni pamoja na kufahamu idadi kamili ya watu wenye viungo hivyo.
 
Ikiwa na watu saba akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Tume hiyo itakuja na majibu yanayofafanua viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika kemikali gani kuvikausha.
 
Pia, jopo hilo litabaini kama ipo sheria na ni ipi  inavunjwa. Wataalamu hao wanalenga kubaini, pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.
 
Kwa mujibu wa Polisi, mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji  eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.