Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed Madulika, mara baada ya kifikishwa nyumbani kwake , Kijiji cha Mikongeni, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro kwa ajili ya utaratibu wa mazishi , Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es Salaam na mazishi yake yamefanyika Augost 8, mwaka huu kijijini hapo.
Baadhi ya Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Majeshi mengine , wakitoa saluti ya heshima ya mwisho mara baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed Madulika, katika makaburi ya Kijiji cha Mikongeni, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro , Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es Salaam na kuzikwa Augost 8, mwaka huu Kijiji hapo.
No comments:
Post a Comment