aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

UTAFITI MPYA KUHUSU KUPOST PICHA MARA KWA MARA FACEBOOK...


Kushare picha kwenye Facebook ni njia ya haraka ya kupoteza marafiki, kwa mujibu wa utafiti mpya
Watafiti wamebaini kuwa wale wanaopost picha mara kwa mara hujiweka katika uhakika wa kukera wengine. Wanaweza kuharibu uhusiano na marafiki, ndugu na wengine wanaoshindwa kwendana vizuri na wale wanaoshare sana picha zao wenyewe.

Dr David Houghton, wa chuo kikuu cha Birmingham cha Uingereza alisema: ‘Utafiti wetu ulibaini kuwa wale wanaopost picha zao kwenye Facebook mara kwa mara wanahatarisha mahusiano yao ya maisha ya kweli. Ni vizuri kukumbuka kuwa taarifa tunazoziweka kwa rafiki zetu Facebook, huangaliwa na watu wa aina mbalimbali, wapenzi, marafiki, watu wa familia, wafanyakazi/wanafunzi wenzako na kila kundi huwa na mtazamo tofauti kwa taarifa tunazoshare.’

 Source:Bongo5

No comments:

Post a Comment