aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

MCHUNGAJI AVULIWA UCHUNGAJI BAADA YA KUONEKANA KWENYE TAMASHA LA RICK ROSS...


Mchungaji Rodney Wills wa kanisa la kibaptisti huko kaskazini mwa Carolina,wiki iliyopita alivuliwa uchungaji huo baada ya kuhudhuria tamasha la Rick Ross
Katika kura zilizopigwa kanisani humo kati ya mashemasi 14. Willis aliambiwa avue madaraka yake baada ya kura za kumwondoa kuwa nyingi jumamosi.
 Kwa umri wake wa miaka 26,Wills alikuwa kijana mdogo sana kanisani kuitwa mchungaji na alipotolewa kwenye nafasi hiyo amekuwa mchungaji aliehudumu kwa muda mfupi pia. Kutokana na taarifa zilizotolewa na AmericanPreachers.com
,Wills alifika kwenye kanisa hilo la Mt Salem jumapili asubuhi na kukuta mizigo yake imetolewa nje na lile bango mlangoni limetolewa.Pia hakuruhusiwa hata kuhudumu asubuhi hiyo.


Miles Langley,shemasi katika kanisa hilo pia alizungumza kupitia website ya wakristo wa kanisa hilo kuwa haikuwa kosa lake la kwanza. Mchungaji huyo huyo alionekana kwenye tamasha la Lil' Wayne miezi 9 iliyopita.

"tunajua kuwa watu wengi watakuwa na maoni mchanganyiko kutokana na matendo yetu,lakini hivi sivyo tunavyofanya mambo yetu katika kanisa la Mt Salem" Aliwaambia wahubiri wa kimarekani. 
"Hatuwezi kuwa na mchungaji anaetukuza mambo ya kidunia dakika hii alafu dakika inayofuata anamtukuza Mungu,basi!"

Kanisa la Mt Salem litakuwa linahudumiwa na wacchungaji wageni mpaka mchungaji mwingine atakapopatikana.

No comments:

Post a Comment