aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 25, 2013

HABARI KUHUSU KULIPULIWA KWA KANISA LA KKKT HUKO SEGEREA,DAR ES SALAAM.


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ushirika wa Segerea limenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kutupa chupa iliyodhaniwa kuwa na mafuta ya taa au ya petroli na kulipuka ndani ya kanisa na kuunguza baadhi ya vitu vilivyokuwemo katika madhabahu ya kanisa pamoja na gari lililokuwa nje ya kanisa hilo majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo.
Itv imefika katika kanisa hilo na kukuta baadhi ya vitu vilivyokuwa madhabahuni vikiwa vimeungua vibaya kikiwemo kitabu kitakatifu cha biblia, huku kukiwa na michanga mingi sakafuni baadhi ya vyombo vya muziki vikiwa vimeparaganyika wakati waumini wa kanisa hilo walipokuwa katika jitihada za  kukabiliana na moto huo usilete madhara.
Akielezea tukio hilo mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Segerea Bwana Noha Kipingu, amesema  limetokea majira ya saa 8 za usiku wa kuamkia leo ,wakati baadhi ya waumini wakiwa ndani ya kanisa katika maombezi ya yaliyoanza saa 4 usiku kwa ajili ya mkutano unaotarajiwa kufanyika jumapili ya agosti 25 mwaka huu.
Akielezea msimamo wa kanisa KKKT usharika wa Segerea kuhusu tukio hilo, licha ya kusisitiza linachukuliwa kama sehemu ya matukio mengine ya ulipuaji wa makanisa yanayoendelea,amesema kwa mujibu wa maelezo ya mlinzi wa kanisa ameona watu wanne waliotega chupa na kulipua kwenye gari la kanisa pamoja na kurusha chupa nyingine ndani na kisha kukimbia.
Baadhi ya waumini walionusurika katika tukio hilo wamesema wamesikia mshindo mkubwa wa kitu kinachofanana na bomu katika madhabau ya kanisa hilo wakati wakiwa wamesimama mbele ua kanisa hilo na kisha moto ukaanza kuunguza madhabau hali iliyowafanya kukimbia na kisha kurudi ndani kwa ajili ya kuzima moto huo.
ITV

No comments:

Post a Comment